Kigoma kwazuka kikundi cha ubakaji kinachoitwa 'Tereza'

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Mji wa Kigoma umekumbwa na fadhaa baada ya kuibuka kwa kundi la vijana ambalo huingia ndani ya nyumba nyakati za usiku wa manane wakiwa utupu wakibeba visu na mapanga na kufanya ubakaji kwa wanawake kwa nguvu.

Hali hiyo imedumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa,ambapo vijana hao wanaojulikana kama “Tereza” kutokana na kujipaka mafuta yanayowawezesha kuteleze wakishikwa,wamekuwa wakiendesha vitendo hivyo hasa katika maeneo ya Katubuka,Bangwe,Mwanga na Gungu ambapo wanawake walionusurika katika matukio hayo wamesema wengi wamebakwa na wengine wanaoakataa kujeruhiwa kwa visu na mapanga na kwamba vijana hao huingia uchi katika nyumba ambazo wanajua kuwa hazina wanaume.

Diwani wa kata ya Mwanga Kusini Mussa Maulid amesema katika kata hiyo zaidi ya wanawake 12 wamefanyiwa vitendo hivyo vya udhalilishaji na kundi hilo ambalo awali watu waliamini kuwa ni ushirikina lakini imebainika kuwa ni kundi la vijana ambao wameanzisha mtindo huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema polisi wameanza msako dhidi ya kundi hilo na tayari mtu mmoja amekamatwa na anahojiwa na polisi kuhusiana na matukio hayo.

 
Hao Mbona rahisi sana kuwasambaratisha? Wakikamatwa wawili tu, wanahasiwa hadharani mbele ya umma uone kama wenzake hawajaacha hiyo Tabia...
siyo kuhasi,unaondoa kabisa abakie na tundu la mkojo tu,
 
kama wanajua kuwa wanajiita hilo jina "tereza" basi wanawajua na hivyo rahis kuwakamata, otherwise waliotendewa unyama huo ndo wawe wamewabatiza hilo jina
 
Back
Top Bottom