Makamanda wa CHADEMA wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kijiji cha Mkabogo ndani ya jimbo la Kigoma kaskazini siku ya Jumapili. Mchakamchaka huu utasimamiwa na vijana wapenda mabadiliko na wazalendo wa kweli wanaoamini mabadiliko ya wana Kigoma kaskazini yataletwa na wana kaskazini wenyewe chini ya viongozi wazawa na sio kama ilivyo kwa mamluki aliyepo. Mkutano utashereheshwa na kamanda Kamsige Mbasa, mhadhiri wa chuo kikuu Mr Akran Yonna,Obama ambaye alikuwa kampeni meneja wa Zitto na utasimamiwa na mwenyekiti na katibu mkoa wa Kigoma.
Mchakamchaka huu umeandaliwa kwa lengo la kumzika mkoloni mweusi wa CCM na vibaraka wake kama Zitto Kaburi na jeneza tayari vimesha andaliwa jambo tunalolisubili ni ibada tu ya mazishi na kuwaimbia wimbo wa parapanda. Karibuni makamanda kote mliko na aminini Kigoma mziki ni mzito, vijana hatulali, morali iko juu na mpango uliopo mwakani CCM hawezi kufufuka kutoka kaburini.