AIR MSAE
Member
- Aug 23, 2016
- 22
- 17
Waziri Ummy Mwalimu kama unavyofahamu sekta ya afya nayo iliingia katika mpango wa BRN ili kuboresha huduma za afya nchini
Mh. Waziri,halmashauri hii ya Kigoma iliingizwa Nov 2015 katika mpango huu na Aug 2016 tukaletewa fungu la 10mil kwa kila kituo cha afya kilichokuwa na mapungufu ili tuweze kurekebisha huduma kwa ujumla
Mh.Waziri hizi pesa zilikwisha kupanhiwa bajeti na wizara tayari na matumizi yake yakaachwa yasimamiwe na wakuu wa vituo husika wakishirikiana na kamati zao za afya za vituo husika
Kilichonifanya nikuombe utusaidie ni kwamba;
-Tangu tumepewa hizo pesa ambazo zimeingizwa katika akaunti za vituo husika,mganga mkuu akishirikiana na mkurugenzi wanaendesha mikakati ya chini kwa chini kwa kukataa tusitoe hizo pesa tukaanza kuboresha vituo vyetu
-Kila kiongozi anayeletwa Kigoma imekuwa ni kuja kuchuma na kuondoka bila kuacha lolote litakalowakomboa wanakigoma
-Kama Magufuli anaamini alituletea mkurugenzi makini katika wilaya ya Kigoma hakika tunayoanza kuyaona kwake bila shaka atakua amejivua nguo kwa huyu mama
-Huyu mganga aliyepo hana sifa ya kukalia hicho kiti maana ndiye amekua mtu wa kwanza kuzuia jitihada za maendeleo katika sekta hii
-Tunaomba pia stahiki zetu zifanyiwe kazi kwa kuwa kila tunapouliza tunaambiwa pesa zetu amejiazima mkuu wa idara,ndipo tunajiuliza huyu mkuu wa idara ni nani bila majibu,hivi kazi tufanye sisi halafu mwingine ajineemeshe je Mheshimiwa hii ni haki?
-Mh. Waziri naomba ufanye ziara wilaya hii ujionee mwenyewe niliyokueleza
-Mh Waziri msitutenge sisi watu wa Kigoma kama vile tumemkosea Mungu kufanya kazi huku,tunakuomba utoke Dar uje napo kututembelea utuone tunavyoteseka
Naomba kwa yoyote aliye karibu na Mheshimiwa huyu anifikishie hii nakala yangu kwa mama yetu huyu wa afya
Watumishi wa afya halmashauri ya wilaya Kigoma tumekata tamaa na kuhudumia wananchi kwa dhuluma na manyanyaso tunayoyapata
Nawasilisha