Hivi hawa wanaoitwa vigogo wanapohama CCM kwenda CHADEMA nako wanatarajia wakawe vigogo au wananchama wa kawaida? Maana nahisi kama CHADEMA kunaweza kukachafuka ghafla hapo baadae hasa baada ya uchaguzi, maana fikiria mwenyekiti wa CCM wa mkoa anapohamia chama kingine amejipanga kwenda kuwa mwanachama wa kawaida au nako anataka akawe mwenyekiti wa mkoa wa chama alichohamia? Na kama ndo hivyo aliowakuta kwenye uongozi je? Ngoja tusubiri tuone. Najaribu kufikiria hata Lowasa atakaposhindwa urais ataendelea kuzunguka mikoani kama Slaa alivyofanya kukijenga chama? Maana naona kama jamaa anataka urais tu akishindwa anasepa zake.