Kigogo CCM Kahama ahamia CHADEMA

Kigogo CCM Kahama ahamia CHADEMA

chaikavu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2015
Posts
760
Reaction score
473

CCM-10August2015.jpg

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kwa ufupi
Ni siku chache baada ya kushindwa kura ya maoni akidai haki haikutendeka, kuhujumiwa

Kigogo mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, mkoa wa Shinyanga, ambaye pia alikuwa akiwania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge wa Jimbo wa Ushetu na kushindwa katika kura ya maoni, ameamua kuacha kukitumikia chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kigogo huyo amekiahama chama hicho pamoja na wanachama wengine 50 wa CCM siku chache baada ya kuangushwa katika kura ya maoni za ubunge, akidai haki haikutendeka wakati wa kampeni na upigaji kura hiyo.

Akizungumza na NIPASHE mjini hapa mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kahama, Juma Protasi, alisema wanachama wa CCM zaidi ya 50 wamejiunga na chama chao akiwamo Bukakiye ambaye alikuwa mweka hazina wa chama hicho tawala wilaya ya Kahama.

Alisema kati ya waliojiunga na Chadema, 12 ni mabalozi wa CCM Kahama mjini na mwenyekiti wa chama hicho tawi la Majengo.

Protasi alisema Chadema kwa sasa kinaendelea kuimarisha ngome zake kwa ajili ya kuandaa mazingira ya ushindi katika majimbo yote matatu wilayani humo ya Ushetu, Kahama Mjini na Msalala.

CHANZO: NIPASHE
 
👍🔒 atatufunga huy6u
hakuna kumchagua tumwache na makufuli yake
 
Hivi kigogo kibakie CCM kinangoja nini wakati mizizi imeshang'oka ,lazima Miccm itambue kuwa hakuna mto Tanganyika kuna ziwa.
 
Hivi hawa wanaoitwa vigogo wanapohama CCM kwenda CHADEMA nako wanatarajia wakawe vigogo au wananchama wa kawaida? Maana nahisi kama CHADEMA kunaweza kukachafuka ghafla hapo baadae hasa baada ya uchaguzi, maana fikiria mwenyekiti wa CCM wa mkoa anapohamia chama kingine amejipanga kwenda kuwa mwanachama wa kawaida au nako anataka akawe mwenyekiti wa mkoa wa chama alichohamia? Na kama ndo hivyo aliowakuta kwenye uongozi je? Ngoja tusubiri tuone. Najaribu kufikiria hata Lowasa atakaposhindwa urais ataendelea kuzunguka mikoani kama Slaa alivyofanya kukijenga chama? Maana naona kama jamaa anataka urais tu akishindwa anasepa zake.
 
Kwanza tuwatoe hawa wezi Oktoba..Chama atakijenga Mbowe na makamanda.
Tunachotaka sasa hivi ni NCHI.Tutavuka daraja tutakapolifikia ndugu Mazingira..
 
Leo upepo umepuliza Dar nyeti zote za kuku zmeonekana bado arusha,mbeya na mwanza
 
Back
Top Bottom