Kigogo CCM alia rafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo CCM alia rafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  Na Elisante John


  Kutuhumiana miongoni mwa wagombea wa nafasi za uongozi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake, kumeendelea kukitesa chama hicho.

  Tuhuma za rushwa zimeibuka katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, baada ya kada mkongwe kulalamika hadharani kwamba anasukiwa mizengwe ili aikose nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa chama hicho.

  Kada huyo ni Mbunge wa zamani wa Iramba Magharibi, Mgana Msindai, ambaye amelalamika hadharani wakati akirejesha fomu zake za kugombea nafasi hiyo.

  Baada ya kurejesha fomu hizo, Msindai alilalamika kuwa anafanyiwa mizengwe kutokana na kuchafuliwa jina lake, akisingiziwa kwamba anataka kutoa rushwa ili achaguliwe kwa kugharimia mikutano ya chama hicho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msindai alisema njama hizo zinaonyesha wazi kuwa zimeandaliwa kwa lengo la kumchafua ili aonekane hafai kuwa kiongozi wa chama chake.

  Kutokana na hali hiyo, Msindai aliyekuwa mbunge wa Iramba Magharibi 1995-2010, alimtaka Katibu wa CCM Wilaya ya Mkalama, Salum Mpamba, kumuomba radhi, kwa kutangaza kuwa atafadhili mikutano ya chama na jumuiya zake ngazi ya wilaya hiyo.

  Msindai alidai kuwa Agosti 28, mwaka huu katika kikao cha CCM Wilaya ya Mkalama, katibu huyo aliwatangazia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya hiyo kuwa yeye (Msindai), atagharimia mikutano yote ya chaguzi za jumuiya ya chama hicho, jambo ambalo alisema siyo kweli na hafahamu chochote juu ya kauli hiyo.

  Msindai alisema kitendo cha katibu huyo kutoa kauli hiyo ya ahadi kwenye mkutano mkubwa kama huo kwa niaba yake (Msindai) bila kuwasiliana naye, kinalenga kumchafua ili aonekane ni mtoa rushwa, hivyo amemtaka katibu huyo amwombe radhi kwa maandishi.

  Hata hivyo, NIPASHE ilipowasiliana na Mpamba kutoa ufafanuzi wa madai ya Msindai, alisema kauli yake haikuwa na nia ya kumchafua mgombea huyo, bali yeye (Mpamba) akiwa kiongozi wa chama, alikubaliana na wenzake kuomba msaada kwa wagombea na wana-CCM wengine akiwemo Msindai kwa ajili ya kusaidia kugharimia chaguzi hizo.

  “Tulikuwa hatujawaandikia barua, lakini tutawaomba wote kuanzia Joramu Allute (Mwenyekiti anayemaliza muda wake) na Msindai bila kujua kuwa na yeye ni miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo ya mwenyekiti wa mkoa,” alisema Mpamba.

  Msindai ni kati ya wanachama sita waliochukua na kurejesha fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania uenyekiti wa mkoa wa Singida katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao. Wengine walioomba ni Allute, Amani Rai, Haruna Kabombwe, Hussein Yusufu na Joseph Saenda.

  Chanzo: Nipashe
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wale Wale wa OLD CCM CULT hakuna WAPYA? Na Wamepewa WILAYA MPYA... Kwahiyo Kutakuwa na MBUNGE MPYA??
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magamba bwaana!Huyu jamaa bado yupo?Mgana msindai!!Anashangaa nini sasa wakati Ccm hii ndo nguzo yao kuu?kama anashangaa hili sasa hivi ataambiwa we chadema maana chadema ndo hakunaga rushwa!!Yeye ajitahidi kufanya uongo na rushwa maana Ccma bdo baba wa huo uongo na rushwa ufisadi wizi na uchafu wote!!Kula shusho Jibaba msindai sijui anakilo ngapi siku hizi fisadi lile 2000 nini?
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mi bado sielewi anacholalamika hapa..rushwa is the name of the game huko ccm...he cant defeat them so he might as well join them
   
 5. I

  IBRAAH Senior Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huwa wanafurah CDM ikichezewa rafu sasa naye yamemkuta analalamika analalamika nn? komaa ukiua kwa upanga na wewe utauwawa kwa upanga.
   
 6. I

  IBRAAH Senior Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haswaaaaaaaaaaa!!! mkuu anajiifanya leo hajui
   
 7. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Magamba bwana hawaishi vi2ko
   
 8. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Yaani hii muzee bado ipo na inahangaikia siasa ?? Huyu enzi zake alikuwa anatesa saana akiwa bwana nyama, tena akipumua tuu swala na palahala kadhaa wanaangushwa...!! Wamekula sana ila kama kawaida ya magamba nyingi zimeishia ktk sketi, na lile limwili kama la Komba sijui kama bado analo...lol Hawa walihonga sana enzi zile within magamba sasa hawakuchelewa kutosana kama kawaida yao..! Sio mpaka mfie ofisini, pumzikeni au kama vipi mwaga hazarani rafu zenu tangu nyuma ili wananchi tuelewe na tuwapige chini magamba kama kumsukuma mlevi....

   
Loading...