Kigoda cha weekend

navin-govind

Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
72
Reaction score
118
Wakuu,

Jana tulipotoka ofisini mimi na mshkaji fulan hivi aliomba nimpe kampani wakati akimsubiri demu wake pale hongera bar. Ahadi yao ilikua ni saa kumi na mbili kamili jioni hapo hapo hongera bar.

Budget ya mshkaji ilikua ni bia tano za kwake, bia tano za demu, na alitenga elfu kumi ya jikoni, halaf elfu ishirini ni nauli ya mwanamke japo anaishi Mwenge Jirani kabisa na hongera bar tulipokuwepo

Huyu jamaa ni mchumi sana japo ana mshahara mkubwa,Tumekaa weee demu haonekani hadi saa moja, Mara Saa mbili kila akipigiwa simu anadai nipo njiani tangu six jioni hadi eight anasema yupo njiani

Saa tatu usiku ndo anaingia hongera bar, wakati huo jamaa keshakunywa bia zote kumi zake na za demu, ile kumi elfu keshaagiza mbuzi tumekula.Iliobaki ni ishirini elfu ambayo aliitenga kama nauli ya mwanamke (nadhan nikisema neno nauli naeleweka)

Demu alipokaa tu kwenye kiti jamaa akainuka akampa elfu ishirini akamwambia si tunaondoka hiyo hapo nauli yako tumesubiri hapa tangu six na nimeshatumia budget yote niliyopanga tuitumie isipokua hiyo twenty

Surprisingly demu alituambia kaeni chini mbona mna haraka? I will take over the cost anzeni upya bill itakua kwangu akasema huku akimwita muhudumu atusikilize. Kwa kweli tulibaki wadogo kama piriton, huku meza za Jirani wakionekana kutushangaa kwa mabishano yaliyotokea.

Hata hivyo bado nashangaaWanawake inakuaje mtu mmepanga muonane saa kumi na mbili unakuja saa tatu usiku?! Unakuja wakati mtu ameshatumia budget nzima maana safari moja uanzisha nyingine, pia sio kila mtu mtumiaji wa hela ovyo.

Wakati weekend inaingia hebu tujadili hili wakuu tafadhali lugha mbaya sio mahala pake pita tu.

Wakuu weekend njema
 
Jamaa yako alionyesha udhaifu sana kukubali kubaki, next time huyo manzi atafanya hivyo tena since anajua akija atamtuliza jamaa kwa kulipia bili zitakazofuata.

Principles and character make a man
 
Kwahiyo midume mizima mmelipiwa na demu ??
 
Reactions: amu
Mmeaibika sana mkajidai mtamkomoa sio, sasa mwenzenu anafika nyie mnanyanyuka ili iweje, huyo jamaa alipaswa kumuuliza nini kimemchelewesha, sio kuondoka kwa jeuri. Kwahiyo mliongeza bia ngapi ngapi? chedhea wanawake wewe
 
Mlitumia hela ya mume mwenzenu alizomaliza kumtoa. Aliona ye Hana hela. Alilipa gharama zenu name bado akabaki na balance siyo yeye wa 20
 
Muda huo demu alikuwa na jamaa mwingine,sasa walivyoachana ndo akaja Hongera Bar.Wanaume sisi tunapangwaga foleni kama kwenye ATM za NMB bila kujijua.
 
Si naskiaga dar huwa kuna fyoleni
au?????
 
jamaa ana msimamo safi sana,aliponiuzi ni kuleta uchumi ktk hela tu wakati kuna muda mrefu sana alipotezewa,hiyo takeover ya bill by huyo mwanamke imewashushia heshima nyie wote wawili..next time be strong
 
Ushasema safari moja huanzisha nyingine. Alianza huko ndiyo kaja kumalizia hapo.
 
Nyie Ni wapuuzi sana yaani mmetumia hela yangu baada ya mimi kumgonga na kumpa hiyo hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…