Kigoda cha mwenge wa uhuru chaibiwa jijini arusha...


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
90
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 90 145

[h=2]Sunday, June 9, 2013[/h][h=3][/h]

[h=3][/h]


KATIKA hali isiyo ya kawaida na inayoashiria uzembe katika ulinzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, juzi kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips katika Kata ya Sekei jijini Arusha, Hamad Rashid (32) aliiba kiti (kigoda) cha kukalishia Mwenge.


Kuibwa kwa kiti hicho kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas. Kiti hicho hutumika kuwekea Mwenge wa Uhuru unapokuwa katika mbio zake nchi mzima.


Tukio la kuibwa na kisha kukamatwa kwa mtuhumiwa lilitokea juzi saa 11 jioni Sanawari eneo la Mataa. Eneo hilo ndilo lilipangwa kwa ajili ya mkesha wa Mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Arusha.


Kufuatia tukio hilo, Kamanda Sabas aliyetafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia tukio hilo, alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo alishakamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda Mwenge pamoja na kiti hicho.


Alisema tukio hilo lilitokea wakati Mwenge huo pamoja na wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine wakiwa katika harakati za kusoma salamu za utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya ratiba ya utangazaji wa ratiba ya mkesha kutolewa.


Alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, alionekana kwa muda mrefu akiwa amesogelea gari lililokuwa limebeba kiti hicho kilichoelezwa na kamanda kuwa kilikuwa cha akiba.


Alisema mara baada ya wizi kijana huyo alikamatwa na katika mahojiano alisema alikuwa anataka kukiangalia tu na kwamba haikuwa nia yake kukiiba na kuomba msamaha.


Hata hivyo alisema polisi wanaendelea kumhoji ili kubaini dhamira halisi ya kukichukua kiti hicho.

Alisema mara baada ya upelelezi wa kesi hiyo, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yanayomkabili ya wizi wa kiti hicho cha Mwenge wa Uhuru.


Mwenge huo wa Uhuru uliingia Arusha Juni 3 mwaka huu ukitokea mkoani Manyara na utakimbizwa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Arusha kabla ya kukabidhiwa kwa mkoa wa Mara Juni 11, yaani Jumanne ijayo.


VIA /freebongo.blogspot.com
 
master peace

master peace

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Messages
1,450
Likes
3
Points
0
Age
39
master peace

master peace

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2012
1,450 3 0
Ni vyema huyo kijana angeiba na huo mwenge kwani hauna faida yoyote hapa nchini. Hivi rasimu ya katiba mpya inasemaje kuhusiana na mwenge huu wa mafisadi.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
90
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 90 145

Masikini kijana wa watu... labda kweli alitaka kujua hicho kigoda kina UMUHIMU GANI kinasafirishwa NCHI NZIMA na KULINDWA...

Na Wamemshika within hrs; Lakini ukiwauliza waliolipua KANISA wako wapi, wanakimbia...
 
Komeo

Komeo

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
2,476
Likes
472
Points
180
Age
29
Komeo

Komeo

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
2,476 472 180
Hamad Rashid haishi vituko.
 
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
15,615
Likes
6,130
Points
280
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
15,615 6,130 280
Kigoda kina ulinzi,raia wanaporwa mali zao na kuuwawa hovyo.bora kijana angeiba na mwenge akawa celebrity kabisa
 

Forum statistics

Threads 1,274,860
Members 490,833
Posts 30,526,125