KIGAMBONI, DAR: Mtoto wa miaka miwili awekwa uvunguni mwa kitanda baada ya kuuawa kwa kuchomwa na kitu cha ncha kali

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kitovuni na kuwekwa uvunguni mwa kitanda nyumbani kwao Kigamboni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula amezungumza na Mcl Digital leo Aprili, 25 na kuthibitisha tukio hilo.

Kamanda Lukula amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi Jumatatu ambapo inadaiwa kuwa binti wa miaka (20) alimchoma mtoto huyo kwenye kitovu kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumficha uvunguni.

“Ni kweli tukio hilo limetokea juzi, aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu. Si mfanyakazi wa ndani kama wengine wanavyodai, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka,’’ ameeleza Kamanda Lukula na kuongeza:

“Sijapata majina sahihi maana nilielekeza niletewe na bado sijaletewa lakini tukio hilo ni la kweli.’’

Kamanda Lukula amesema baada ya huyo binti kufanya tukio hilo aliondoka nyumbani hapo.

“Huyo binti baada ya kufanya hilo tukio alikwenda kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani,’’amesema

Baada ya uchunguzi wa polisi, binti huyo alikamatwa na alikwenda kuwaonyesha alipomuweka mtoto uvunguni mwa kitanda.

Kamanda Lukula amesema kwa sasa taratibu nyingine za kisheria zinaendelea baada ya mtuhumiwa kukamatwa.

Chanzo; Mwananchi
 
Hapo kaacha mbegu ya chuki kati ya ndugu na ndugu
Huyo binti kweli kichaa
 
Haya yamejiri Kigamboni baada ya dada mmoja kumchoma kisu cha kitovuni mtoto wa miaka miwili na miezi miwili na baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuchukua mwili wa mtoto na kuuficha uvunguni mwa kitanda.
 
Shukrani kwa taarifa lakini je, hii ni tetesi au habari kamili. Vipi kuhusu chanzo cha habari?
 
Toa taarifa kamili au umesikia juujuu clauds fm unakurupuka kufungua uzi
 
Huyo mtoto ni wa kwake au wa jirani? Na je, sabb ni nini mpaka kufanya tukio hilo? Hebu jazia nyama kweny uzi wako.
 
Huyo mtoto ni wa kwake au wa jirani? Na je, sabb ni nini mpaka kufanya tukio hilo? Hebu jazia nyama kweny uzi wako.
Mtoto ni wa ndugu yake. Ni kwamba mama mwenye nyumba alivyokuwa akienda job basi muuaji humleta bwanake na kutombana mbele ya mtoto, sasa katoto kakaiga ile tabia na kuanza kuifanyia majaribio kwa watoto wenzie. Baadae yule mtoto alikanywa na ***** na alivyoulizwa kajifunzia wapi katoto kakasema kwa dada. Yule mama akamkaripia dada na kusema asigeuze nyumba kuwa gesti. Yule dada ndo akakaua katoto. Siku ya kutekeleza mauaji aliongeza sauti ya woofer mpaka majirani wasisikie kilichokuwa kikiendelea.
 
Nimekuelewa mr. Huyo mwanamke sehemu yake ya ubongo itakuwa imeoza. Yy anafikiri akimuua mtoto yy atabaki uraiani? Maisha yake yote anamalizia gerezani.
Aiseee
 
Huyo binti kachotwa na mapenzi ya utoto akawa na akili kama nyumbu. Mbaya zaidi ni ndugu wa hiyo familia kabisa.
 
Back
Top Bottom