Kigaila, ulishindwa na Cheyo, Rais Magufuli utamuweza?

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Nilipomtazama na kumsikia juzi kati hapa, Benson Kigail, kupitia vyombo vya habari akitangaza siku 14 za chama chake, Chadema kwa hakika kabisa mwanasiasa huyo kinana alinirejesha nyuma kama miaka 15 iliyoita hivi.

Katika miaka hiyo 15 na ushee hivi Kigaila alikuwa mwanasiasa kijana mtiifu kweli kwa mwenyekiti wa UDP taifa, John Memose Cheyo na chama chao enzi hizo, Kigaila akiongoza kurugenzi au idara ya vijana ya chama hicho.

Kigaila na kijana mwenzake wakati huo Amani Nzugile Jidulamabambasi (Mwenyezi mungu ampe mapumziko ya amani) ndio waliokuwa nguzo yam zee Cheyo katika miaka ya mwishoni mwa tisini. Walitoa jasho jingi kuijenga na kuitangaza UDP, kuanzia iliposajiliwa tu mwaka 1992 hadi mwaka 2000.

Kigaila na Jidulamabambasi, walikuwa vijana waliokuwa wakiamini katika uafrika zaidi (Pan Africanism), wakiwa wamelishwa na kumeza itakadi ya ujamaa asili wa Afrika, iliyokuwa imeanzishwa na kusimikwa na Kiongozi wa Libya wakati huo Kanali Muammari Gadafi, kupitia kitabu chake cha Kijani (Green Book), walikuwa ni moto wa kuotea mbali wakati ule wa kueneza sera za UDP, wakati huo kikiwa chama pekee chenye nguvu maeneo ya kanda ya ziwa na kidogo kanda ya kati anapotoka Kigaila.

Wahenga hawakukosea pale waliposema shukrani ya punda ni mateke. Mwishoni mwa mwaka 1999 na mwanzoni mwa mwaka 2000, vijana hawa wawili kwa kuungana na wenzao ndani ya UDP, ghafla walimuasi mzee Cheyo kwa kumpindua katika nafasi yake ya uenyekiti wa UDP, kabla ya kuifutilia mbali kamati kuu yake na kujiundia ya kwao.

Mzee Cheyo hakuamini kilichotokea. Na kama angekuwa na ugonjwa wa moyo basi asingeweza kustahimili vituko matukio na vitimbi alivyokuwa akifanyiwa na vijana wale wawili, bila shaka angefariki ghafla kutokana na misukosuko ya vijana aliyoipata wakati akiongoza mkutano mkuu ambao hatimaye ulilazimika kung’oa pale katika ukumbi wa Key’s Hotel Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Enzi hizo, vijana hao kina Kigaila na Jidulamabambasi walikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na kiongozi wa Libya katika harakati zao za kueneza Itikadi ya Ujamaa wa kiafrika zaidi katika bara lote la Afrika, Gadafi wakati ule alikuwa na ndoto na malengo ya kuitawala Afrika chini ya mwamvuli wa mataifa ya Afrika yaliyoungana (Afrikan United State-AU).

Naamini mpaka sasa Mzee Cheyo anamshukuru sana, Msajili wa vyama vya siasa nchini, enzi hizo Jaji John Bill Tendwa asingekuwa upande wake, vinginevyo mwanasiasa huyo mkongwe nchini na mbunge wa bariadi kwa siku nyingi angekuwa ameshasahaulika katika ulingo wa siasa nchini.

Pengine kwa kutumia uzoefu wake, weredi na taaluma ya sheria wa ngazi ya Ujaji, Tendwa aliweza kung’amua kuwa chanzo cha mapinduzi hayo ni ruzuku hivyo akaumaliza mgogoro kwa kukataa kuutambua uongozi wa uasi huo wa kina Benson Kigaila.

Baada ya msajili kung’amua kuwa tatizo ni ruzuku kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi ya kina Marando na Mrema alichoamua ni kuwanyima ruzuku akina Bensoni Kigaila badala yake akawa anaendelea kumpa ruzuku mzee Cheyo, hivyo Kigaila na Jidulamabambasi na wakaamua kuachia ngazi na kuenda katika vyama vingine na hapo ndipo mwanzo wake wa kuelekea Chadema ulipoanzia.

Nakumbuka Jidulamamabasi aliamua kurudi CCM na yeye Kigaila aliamua kwenda Chadema amabapo kwa sasa anatajwa kama Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Operation za chama hicho.

Binasfi naamini kama Mbowe na wenzie wangejishughulisha kidogo tu kutaka kumfahamu historia zaidi Kigaila, wasingethubutu kumtwisha madaraka makubwa hayo ambayo yanamfanya aweze kuingia mpaka jikoni kunako mikoba ya chama chao, kwa sababu ni kijana hatari kimkakati.

Ndugu zangu, haikuwa nia yangu kukumbushia yote hayo lakini niliamua kuanza na utangulizi wa historia ya Kigaila ambaye anatajwa kama kuwa Mkuu wa Mafunzo na Operation wa chadema kwa kuwa nataka kuijadili siku 14b alizozitangaza kuanzia June 4 ambazo aliziita siku chungu kwa serikali ya Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi.

Sijui hizo siku 14 zimeleta adha na uchungu gani kwa Serikali ya Rais Magufuli na CCM kwa ujumla wake, kama alivyotangaza Kigaila katika vyombo vya habari na kupewa kurasa za mbele katika magazeti yao, akiwa makao makuu ya Chadema pale mtaa wa Ufipa Kinondoni, Dar es Salaam, kwa lengo la kutangaza kile ambacho magazeti yao ya propaganda yaliandika “ Siku 14 chungu kwa CCM”.

Tangu June 4 mpka sasa ni zaidi ya mwezi mmoja takribani na nusu, hatujaiona operationi hiyo ya siku 14 ambayo tuliambiwa itaongozwa na Lowassa, Sumaye na Mbowe pamoja na Dr.Mashinji popte pale nchini au hatujui imeyeyukia wapi?

Bwana Kigaila alipaswa kuja tena mbele ya waandishi wa habari na kutuambia mafanikio na changamoto za hizo siku 14 alizozitaja mbele ya kamera za waandishi lasivyo aache kuuhada umma kwa habari zake za propaganda za kutaja siku ambazo hatuoni operationi yeyote iliyofanyika zaidi ya siasa za kitoto za Bavicha.

Naomba kutoa ushauri wa bure kwa Kigaila ikiwa alimshindwa Mzee Cheyo enzi zile za UDP, kamwe hata muweza Rais Magufuli na Chama chake ambapo muda si mrefu atakabidhiwa kijiti na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dr. Jakaya Kikwete ili kukiongoza chama hicho.

Nitoe pia angalizo kwa Kigaila na wanasiasa wakurupukaji na waropokaji kwa lolote linalowajia vinywani mwao kwamba hizi zama ni za Magufuli, kwa mwanasiasa yeyote makini ili aendelee kudumu katika maisha yake ya kisiasa, ni bora akachagua kuungana na Rais Magufuli, vinginevyo, akienda, kinyume chake anajichimbia kaburi lake la kisiasa yeye mwenyewe.

Mwisho Kigaila amuangalia Msingwa pamoja na machepele yake yote na uropokaji wake lakini tulimuona akiwa amejisalimisha kwa Rais Magufuli wakati wa ugawaji wa madawati kwa majimbo yote ya wabunge, licha ya tangazo la chama chake kuwataka madiwani na wabunge kutoenda katika shughuli zozote watakazoalikwa na serikali na hiyo ilitokea baada ya diwani mmoja wa chama hicho kuhudhuria katika mkutano mmoja ulifanyika katika viwanja vya Biafra kinondoni ambapo aliitwa na Rais Magufuri kuja kusalimia wananchi.
 
Back
Top Bottom