Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,004
Naam jicho la tatu limeshachungulia wanaChadema kindai ndaki wameshaamka sasa ni wazi wazi wantamka maneno makali yenye kuonyesha kutoridhishwa na uwepo wa Lowassa ndani ya chamn na upande mwingine wa shilingi yaani Team Lowassa wao wanajipanga na wameweza kupandikiza watu wao katika vikao vya maamuzi, naaum mbegu imepandwa na imeota sasa inamea, naaaum mmea wenyewe ni miba mikali sasa inachoma.
Kwa 'makamanda' Lowassa si tena raisi wa mioyo yao kama walivyomwita Dr.Slaa kwa miaka mitano mfululizo kabla ya kurubuniwa mwaka 2015 lakini kwa teamLowassahuwaimbii kitu. Kwa haraka haraka nyufa nyingi zimetokea kiasi kisichoelezeka na huenda 'jumba' likalemewa na kuanguka.
Naaam, 'ajizi nyumba ya njaa' kama ambavyo waswahili walivyonena..kwa sasa Zitto ameonekana kufurahiwa na 'makamanda' wakijuta sasa kumpoteza, kila mtu sasa anafutilia kauli za Zitto kwenye mitandao na mikutano na kuhakikisha zinasambaa kwa watu wengi wakati huohuo 'makamanda' wamelaani tabia ya Mbowe kuwachagulia viongozi kwenye kanda za kiutawala ndani ya chama hadi kupelekea makumi na mamia ya viongozi wa mashina kufa moyo na baadhi kujiuzuru. Kuelekea uchaguzi ndani ya chama na hata uchaguzi mkuu mwaka 2020 njia ni nyeupe na ninawaona baadhi ya wabunge wa sasa wa Chadema haswa wale wasiotokea kanda ya kaskazini na wanachama waandamizi wakihamia ACT Wazalendo na kuendelea na harakati zao kisiasa wakimsusia chama ndugu Lowassa na Mbowe.
Na chakufurahisha zaidi kafulila atagombea ubunge huko Kigoma mwaka 2020 kupitia ACT wazalendo na si Chadema ni suala la muda tu.
Nawasilisha.