Kifo ni Ndoto Endelevu ya Milele

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Kwa lazima kutambua kuwa "ndoto ni maisha ya rohoni" yawe mabaya au mazuri lakini yanategemea sana matendo yako na mind set yako juu ya matendo.

Siku zote matendo mabaya hupelekea ndoto mbaya sana na ukiwa na matendo mema mara nyingi utaota ndoto nzuri na sometime unaweza ukawa unacheka kabisa huku umelala au kulia kabisa. yote hiyo inategemea umeishije siku hiyo na hasa ulikuwa na mawazo gani (positive or negative).

Vitabu vya dini huwa vinasema tunafanya dhambi hata kwa mawazo( mind set) zetu na hivyo ni kujiandaa kupata adhabu za ndoto kuwa mbaya au nzuri.Katika mawazo tuna uwezo wa kufanya mema au mabaya yatakayotuhukumu tulalapo.

Pili tambua "ndoto hutokea usingizini" na "usingizi ni nusu- kufa" hivyo kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kifo na ndoto.yani katika usingizi ufahamu unapotea lakini unapumua na hivyo unaishi maisha(unaonja maisha) ya rohoni kwa maana ya nusu kufa.

Mtu anapokufa tu, anabadili maisha na kuishi maisha ya rohoni ambayo ndiyo ndoto endelevu za milele.kwa kuwa ndoto zina uhusiano wa moja kwa moja na matendo na mind set basi baada ya kufa tu" kama ulikuwa unatenda mabaya tegemea ndoto endelevu yako itakuwa mbaya (jehanamu) na kama ni mema basi utakuwa na ndoto endelevu nzuri (peponi)"

Tambua kuwa binadamu tuna share the same feelings ndotoni na uhalisia.yani ukipigwa ndotoni utaumia sawa tu na ukipigwa katika hali ya kawaida( uhalisia).

Hivyo kitendo cha kufa ni mwanzo wa maisha ya ndotoni.

Hizi theory kwamba kuna kuhukumiwa baada ya kifo ni uongo bali utajihukumu mwenyewe kwa kuteseka involuntarly bila kuwa na msaada.

Kwa leo niishie hapo, nitakuja kuelezea mada nyingine "pepo na jehanamu ni hii hii dunia lakini tunatofautiana yani kila mmoja anayo yake"
 
Ndoto hujengeka kwenye ubongo nivipi MTU ataota ubongo ukisha oza??

Ndoto mbaya Mara nyingi huwa ni zakuhusu, majinamizi na nzuri huwa niza ngono. Nakutokana na mfumo wandoto ulivyo , kwamba MTU huota alicho kuwa akikiwaza kabla ya ndoto jee nikiwaza ngono sana mambo yangu yatakuwa mema baada ya kufa?.
 
Ndoto hujengeka kwenye ubongo nivipi MTU ataota ubongo ukisha oza??

Ndoto mbaya Mara nyingi huwa ni zakuhusu, majinamizi na nzuri huwa niza ngono. Nakutokana na mfumo wandoto ulivyo , kwamba MTU huota alicho kuwa akikiwaza kabla ya ndoto jee nikiwaza ngono sana mambo yangu yatakuwa mema baada ya kufa?.
Haya ni mambo ya rohoni zaid kuliko kimwili. Kiimani ndoto ni zaidi ya kazi ya ubongo kama ujuavyo. Hata hivyo jaribu kupata ushuhuda kwa watu waliozimia kwa muda mrefu ( yaani wengine huzimia kuanzia saa moja hadi siku 1 kabla ya kuzikwa wanazinduka).ukishindwa kuamini Jiulize misukule inafanyeje kazi huku mwili ulioza na mlizika tayari.
mind (soul) does not die forever.
kuhusu "et ndoto nzuri ni ngono'' hapana zipo nzuri zaidi ya hizo. hizi tunazoota ni fupi na zinareflect nini umefanya na mind set ya siku moja.lakini kifo kinareflect maisha yako yote.
unaonekana unapenda sana ngono basi kama muislamu kamili utaota unawatoa ubikira wanawake 72.....(its a joke)
 
Mtu anapokufa, hayupo tena. Kifo ni kinyume cha uhai. Wafu hawaoni, hawasikii wala kufikiri. Hakuna sehemu yoyote ya mwili wetu inayoendelea kuishi baada ya mwili kufa.

“hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi.” (Mhubiri 9:5, 6, 10) Vivyo hivyo, andiko la Zaburi 146:4linasema kwamba mtu anapokufa, “mawazo yake hupotea.” Sisi hufa wala hatuendelei kuishi baada ya mwili kufa. Maisha yetu ni kama moto. Unapozimika,hauendi popote. Haupo tena.

Kifo ni usingizi mzito usio na ndoto.
 
Back
Top Bottom