Kifo cha Nyaulawa na tovuti ya Majira

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
883
I was just wondering kama hawa jamaa wa Business Times wameamua kumuenzi Marehemu Nyaulawa kwa "kuua" tovuti yao!

Hivi ni lini vyombo vyetu vya habari vitapata akili ya kuelewa kwamba tovuti zao ni sehemu yao muhimu?Redio takriban zote "zimeigomea" teknolojia ya mtandao with exception ya Radio Maria.Hata hao wanaojiita wajanja wa mjini,Clouds FM,nao wamechemsha baada ya kuwa hewani kwa kipindi kifupi almost a year ago.TV ndio kabisa.Jump TV inaonyesha stations za nchi nyingine tu.

Back to tovuti,wakati Mwananchi na Tanzania Daima wamekuwa hawaeleweki vizuri as to muda gani hasa wana-update tovuti zao,Daily News na dada yake Habari Leo wana tabia ya kupotea hewani nyakati za alfajiri kwa mida ya hapa.Habari Corporation walichemsha zamani kama Uhuru.Kwa weekly papers,Raia Mwema wanapitisha angalau siku nzima kabla hawajaweka habari mpya.

IPPMEDIA wanastahili pongezi kwani wanajitahidi sana ku-update tovuti yao japo nyakati nyingine unaweza ku-click link ya habari na usiikute.Jamaa ambao wako consistent sana na kuhakikisha tovuti yao inakwenda na muda ni Global Publications.

Wana-JF mlio kwenye vyombo vya habari naomba mtufikishie kilio chetu sie tunaotegemea zaidi online versions za magazeti yetu kupata habari za nyumbani.Wakitaka,inawezekana!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom