Another "verbal diarrhea" from Chagonjwa!!!
wameunda tume nyingine kuchunguza kifo? fu@#$!
Ipo Star TV kweli? Mbona sioni hapa online? Au ni Channel 10? Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE
Wakati umefika kwa jeshi la polisi kutafakari upya mbinu yao ya kuzuia kuenea kwa matawi ya vyama vya upinzani hapa nchini na hasa chama cha CHADEMA. Haiingii akilini kuwa matukio haya ya polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kuzuia harakati za kisiasa za CHADEMA kujitanua na kusambaa kwa kufungua matawi na kuelimisha sera zake ni AKILI ZA KIPOLISI.
Katika mazingira ya kawaida inaonyesha kuwa jeshi letu la polisi ama linatumwa na serikali chini ya maelekezo ya CCM au baadhi ya viongozi wa polisi ni wanachama wa CCM na wanataka kujijengea ujiko ili watunukiwe vyeo ndani ya CCM au serikalini.
MAONI YANGU:
Wakati umefika kwa polisi kutambua mali ni kodi ya wananchi wote bila kujali itikadi ya siasa na rasilimali zote za nchi ni zetu wote kwa manufaa yetu wote. Wajibu wa polisi ni kulinda wananchi wote na mali zao kwa haki na usawa wakiwa wamelala, wanatembea, wanacheza, wanaandamana, wanaelimishana kwa njia ya mikutano, mihadhara au kwa burudani.
Polisi wangejijengea heshima kama wangehakikisha wanatoa ulinzi uliotukuka kwa CHADEMA katika harakati zake za kisiasa za kujitanua, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha wananchi kujua haki zao, wajibu wao na kulinda rasilimali za nchi yao.
Mkuu ni kweli ipo siri, nadhani polisi hasa wa kada ya chini wana agenda yao dhidi ya wakuu wao na serikali pia, kwa kuua raia waio na hatia, wanataka serikali ichukiwe na jeshi la polisi lichukiwe na wananchi , kitu ambacho wameshafanikiwa sana katika agenda hiyo. Imefika wakati sasa viongozi wa pilisi na serikali kukaa kuangali hayo badala ya kuendelea kutupa sababu zisizo na mshiko. Fuatilia matukio ya polisi kujiua, kuwaua wenzao na haya yote utaona kuna kitu, kuna agenda ya kufanyia kazi. Nabaki na imani na JWTZ lakini si Polisi katika kulinda wananchi.Inanikumbusha pia enzi za Soweto, askari wa makaburu ndio waliokuwa wakisababisha fujo na mauaji na si wananchi, hii ndiyo inatokea sasa hapa kwetu. Tusiishie kusema MUNGU IBARIKI TANZANIA, tujiulize aibariki katika lipi.Nimesoma habari hii kwenye gazeti la Tanzania Daima na imenishtua sana, kwamba watawala wameamua kufanya lolote lile ilimradi wawazuie Chadema, soma baadhi ya paragraph hapa chini;
"Alipofuatwa na kuombwa awazuie askari wake kumshambulia mwandishi huyo, kamanda huyo alifunga vioo vya gari lake, akapiga honi mara kadhaa, na akaondoka. Baada ya RPC kuondoka eneo hilo, ndipo bomu lilirushwa na kumfumua mwandishi utumbo."
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Michael Kamuhanda, alisema awali kwamba anaipenda kazi yake, hivyo hawezi kuruhusu mikutano katika mkoa wake mpaka atakapopata maelezo ya ziada.
Alisema: "Ni kweli jana saa mbili tuliwapa barua ya kuruhusu shughuli zao ila hili ni agizo na mimi ninakaribia kustaafu na kazi yangu ninaipenda, hivyo siwezi kuruhusu maandamano kinyume na maagizo yaliyopo."
Alisema CHADEMA hawawezi kufanya mikutano kwa kuwa hawana jeshi wala vifaa vya kupambana na Jeshi la Polisi, hivyo wakijaribu kutotii sheria ni lazima washurutishwe.
Source; Tanzania Daima; Polisi waua tena kikatili
Maundumula tume ipi ambayo imeshawahi kuundwa hata tanzania na ikaja na jibu la uhakika
Unategemea nini mwenye tume akiwa ashatoka na majibu yake ambayo anayasema hadharani
Chagonja alisema waliofanya fujo songea ni wahuni na tume iliundwa ambayo mpaka leo hata majibu hakuna.
Huwa naona ni ulaji mwingine tuu unafanyika kwa hao wanaoteuliwa kwenye hizo tume
m
Penye red unauliza majubu, Unakumbuka Tibaigana akiwa madarakani alisema yeye si mwanachama wa Chama chochote na hashabikii chama chochote? lakini alipostaafu akataka kugombea Ubunge kwa ticket ya CCM kama mwanachama Mkongwe
Mi simo katika maneno ya police Mungu nisamehe kama nimeyasikia kwa bahati mbaya kwani halikuw kusudio langu kusikiliza uongo ule
Kwahiyo anafikiri akistaafu ndio mwisho?Lisu alisema
Wawe wamevaa magwanda au wamevua hawataachwa.Anaelewa
Maana ya huo ujumbe?
Akihojiwa na kituo fulani cha redio kwa njia ya sim leo hasubuhi, kamanda kamuhanda amesema kuwa mwandishi huyo ameuwawa na mlipuko uliotokea kusiko julikana, na amevilaumu vyombo vya habari kuripoti habari zisizo za kweli tofautitofauti, amesema ripoti kamili ataitoa leo baadae.
nawasilisha.