Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwaka 1987 wakati wa mkutano mkuu wa CCM kule Kizota Dodoma, mwanachama mmoja wa CCM alimuuliza mmoja wa wale waliokuwa wanataka uongozi kama anazijua kanuni za msingi za CCM. Mwalimu Nyerere akaingilia kati na kumkejeli muuliza swali, huku akisema kuwa swali alilouliza halipaswi kuuulizwa katika ukumbi wa mkutano. Wajumbe wote waliokuwa ukumbini wakamcheka muuliza swali.
Lakini nyuma ya lile swali kulikuwa na ujumbe mzito sana. Hoja ya muuliza swali ni kutaka kujua kama wote wenye kutaka uongozi kwenye chama wanaunganishwa na nia moja na wanachama wote waliobakia. Umuhimu wa mwana CCM kuwa tayari kuzifahamu kanuni za msingi za chama chake, umekuwa ukipuuzwa sana ndio maana bila hata ya aibu baadhi ya wanachama hawakuona taabu kuanzisha mitandao ya kirafiki ndani ya CCM.
Wanachama wa CCM waliipuzia misingi inayowaweka pamoja kiasi cha kuwa tayari kuigawa nchi kwa sababu za kibinafsi. Na zipo habari kuwa ni tangu enzi zile za miaka ya 80 mwishoni, ndipo hawa watafuta urais waliopigwa chini mwaka jana, walipoanza kutengeneza makundi ya watu watakaowaunga mkono mbeleni. Rais wa awamu ya tano ambaye inaaminika kuwa hakuwa na wafuasi wa siri, anayo bahati ya kuongoza nchi wakati yale makundi yenye tamaa mbaya yakikosa nguvu na hamu ya kuendelea kujiweka sawa kwa nia za kupata madaraka. Labda yaibuke makundi mengine miaka ijayo.
Na aitumie vizuri bahati hiyo kwa kuendeleza uadilifu ili CCM irudi kwenye zile enzi za mtu kujiunga na chama kwa sababu ya itikadi na sio kwa sababu ya kutaka kuganga njaa. Ni mambo yanayowezekana kutekelezeka, wala sio njozi.