Kifo cha mahaba

BRN

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
5,476
Reaction score
7,029
....kina idhilali..hakina haiba wala afadhali.. Bali tajikaba nifilie mbali... Kufa kwa mahaba ni adhabu kali.. Leo ni msiba usio mithali... Kesho ni adhaba mbele ya jalali.. Eeewe mahabuba niepushe hili. Ni wewe tabiba hapana wa pili... Napanda jasba tajiua kweli....... Ni maneno ya Bi.Shakila hayo..je tujiulize na kutafakari maneno yake..hatuyaoni leo yakitokea!?
 
mpangilio wa beti muhimu...
 
mpangilio wa beti muhimu...

Nilizipanga lakini kwa vile natumia simu ya mkononi jf imeziunganisha..pole kwa usumbufu ulioupata.
 
dah naomba nihakiki hilo beti...
mtindo_katumia wa kimapokeo maana unavina na mizani.

muundo_mpangilio wake wa mashaili sio wa moja kwa moja kwani amechanganya matukio.

matumizi ya lugha_amejitahidi kutumia tafsida.pia kuna tamathali za semi...

maudhui..dhamila kuu...mapenzi.

dhamila ndogondogo..kifo kinavyowezwa kusababishwa na mapenzi .uaminifu..

migogoro..mgogoro wa kinafsia......

uwiiiiiiiiii.sijui nimepatia..ngoja wengine waongezee na kukosoa..
 
si kweli hata ushairi wa wana usasa unakuwa na beti. ingawa beti hizi zinaweza kuwa na mistari ambayo hailingani.
akisema ametumia mtindo wa wana usasa yuko sahihi
 

umenikumbusha mwalim wa kiswaz
 
Hapo alikuwa akizungumzia mapenzi ya dhati, mapenzi ambayo hayajajengwa juu ya msingi wa fedha, gari wala nyumba kwa maana vyote hivyo huja na kupita kama ambavyo maua hunyauka na kuchanua. Hapo alikuwa akizungumzia mapenzi ambayo msingi wake ni uaminifu na uwajibikaji. Ndio, ni lazima uwajibike kwa yule umpendae ili kulinda mustakabali wa penzi lenu... Habari zenu wanajf hususani mmu, ni mgeni wenu mie nahitaji kujumuika nanyi mahali hapa.
 
Karibu sana
 

Uko vizuri mkuu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…