Kifo cha Leopold Lwajabe dhidi ya uongo wa Mambosasa: Aibu dunia nzima "skunk of the world"

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
6,054
5,432
MAMBOSASA AMEIBUA MASWALI MAGUMU 12 KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Juzi niliandika kuwa Leopold Lwajabe, aliyekuwa Mkurugenzi wa miiradi ya Umoja wa Ulaya nchini (EU) katika Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye alikutwa ananinginia mwisho wa wiki, kabla ya kifo chake alilazimishwa kuandika wosia, wahusika wakauchomkea ofisini kwake kwa siri ili kuficha mazingira ya kifo chake.

Leo jioni nimemsikia Lazaro Mambosasa, Kamanda za Polisi Kanda ya Dar es Salaam, akithibitisha andiko langu kwa kulitokea maelezo, hasa kuhusu WOSIA. Mtu yeyote anayejua saikolojia, anaelewa kwanini Mambosasa amejitokeza kuzungumzia wosia huo.

Katika andiko langu la awali lililosambaa kwenye mitandao ya kijamii nilisema:

INASIKITISHA: YA NDANI KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Dotto James, Katibu Mkuu Hazina (mpwa wa Raid Magufuli) ambaye ni bosi wa Leopold Lwajabe anatuhumiwa kuwa na mkono katika sakata la kifo cha LWAJABE.

Juzi kabla mwili haujapatikana Dotto alikuwa na vikao vya siri na polisi wasio na sare kujadili statement waliyopika kuhusu marehemu. Yeye alijulishwa kifo Jumamosi usiku, na Jumapili alishinda na hao polisi.

Lwajabe alikuwa akilalamika juu ya watu wanaomfuata kutaka hela za kitengo cha EU hapo wizarani. Alipokataa walimtisha kuwa wanamjua kila kitu na kuwa yeye ni raia wa Rwanda.

Katika kipindi hiki cha kuhangaishwa kwake, familia yake huko Karagwe ilihojiwa na maafisa usalama kuhusu uraia wake mara kadhaa.

Alipotekwa mara ya kwanza wiki moja iliyopita, alisainishwa makaratasi ya ofisi na kisha akalazimishwa kuwapa password ya ATM card na fedha zake zikachukuliwa zote.

Alirudushwa na gari la Noah na kutupwa jirani na kwake Kinyerezi. Waliomrudisha hawakutaka kujulikana. Gari jingine liliendelea kuzunguka eneo hilo kwa siku mbili kuchunguza kina nani wanafika na kutoka.

Yeye alikuwa kama amechanganyikiwa na akawa anatoa hadithi zinazojichanganya. Mwenyewe alitishwa kuwa akisema yaliyomtokea watarudi kummaliza. Wamemmaliza kimya kimya! Alipotekwa mara ya pili, wiki hii iliyoisha juzi, polisi waliendelea kuwatuliza ndugu zake kuwa ataonekana ndani ya saa 72, wakawaonya wasisemeseme sana.

Chanzo kutoka ofisi ya ZCO kinadai watekaji wake si polisi ila ni watu wenye nguvu waliokuwa wanawaagiza polisi mambo ya kufanya. Lwajabe alifanyiwa unyama mkubwa. Alilawitiwa na kupigwa picha. Alilazimishwa kuandika barua kuwa amejiua kwa sababu ya matatizo yake binafsi na kwamba asilaumiwe yeyote. Alilazimishwa kuandika wosia na ukapelekwa na kuingizwa ofisini kwake. Wauaji walimfunga kamba na kumtupa kichakani Mkuranga.

Kisha waliwaelekeza polisi waende kuchukua mwili na kuuweka hospitali. Polisi hawakwenda na camera kuchukua picha za eneo wala kuchukua alama za vidole mwilini. Mmoja wa wapelelezi ni ndugu ya marehemu, na alipogundulika polisi walisitisha jitihada zote za kupika ripoti. Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna kundi maalumu la siri serikalini lipo juu ya kila taasisi, na linachotaka ni fedha. Ni ujambazi wa kidola. Inasikitisha sana!

MASWALI YANAYOIBULIWA NA MAMBOSASA:

Kauli ya Mambosasa kuwa Lwajabe alijiua na aliandika wosia huo uliokutwa ofisini mwake, imethibitisha nilichoandika awali, na imeibua maswali mengine kadhaa.

Hapa naweka maswali 12 ya msingi ya haraka haraka ambayo Mambosasa angepaswa kuyajibu:

1. Mtu ambaye ameshaamua kujiua kwa kujinyonga mtini, hadi anaandika wosia na kuuacha ofisini, kwa nini atoke Dar es Salaam asafiri na kupita miti yote hadi Mkuranga, huku nyumbani kwake Kinyerezi kumejaa miti ya miembe ambayo ingemfaa kwa jambo hilo?

2. Lwajabe aliondoka nyumbani kwake akiwa amevaa shati. Amekutwa mortuary Mkuranga akiwa na tisheti. Kama Mambosasa ni mkweli, kwa nini hadi sasa dereva wake, karani wake na ndugu zake hawajahojiwa juu ya mabadiliko haya ya mavazi?

3. Kwanini polisi waliamua kumuondoa eneo la "kujinyongea" na kumpeleka mortuary bila kuita ndugu zake, wakati walikuwa na RB namba za kupotea kwake? Walikuwa na haraka ya nini?

4. Kwanini polisi hawakutumia forensic equipments ili kurahisisha uchunguzi?

5. Kwanini polisi hawakutaka ndugu wa marehemu kushiriki katika post-mortem na kwanini hawakuwapa taarifa za awali za uchunguzi?

6. Kwanini serikali ilijua wosia wa marehemu kabla ya kifo kutangazwa. Kwa nini polisi walikuwa wanamtafuta marehemu mezani kuliko vichakani?

7. Kabla ya kifo chake, kwanini maofisa usalama mkoani Kagera walisumbua familia yake na kuchukua maelezo yao baada ya Lwajabe kutekwa mara ya kwanza? Kwa nini mdogo wa marehemu aitwaye Meneja Byase alihojiwa na TISS kipindi marehemu ametekwa mara ya kwanza? Walihoji kuhusu nini, na mbona Mambosasa hasemi haya?

8. Kwanini Katibu Mkuu Hazina, Dotto James, alikuwa anamlazimisha Lwajabe aende likizo ya wiki mbili baada ya kuwa ametekwa mara ya kwanza?

9. Kwanini askari wa Kikosi Kazi (Task force) wasichukuliwe alama za vidole ili kulinganisha na alama za vidole kwenye baadhi ya vitu vilivyochukuliwa na askari aliyewatoroka na akaviacha kituo cha polisi Mburahati?

10. Kwanini polisi walikazana kutaka ndugu wa marehemu wasisemeseme na kwamba ndugu yao angeonekana ndani ya saa 72 baada ya kutekwa? Walijuaje? Lengo lao lilikuwa nini?

11. Kwanini Katibu Mkuu Dotto alizuia kifo cha Lwajabe kutangazwa Jumamosi jioni wakati mwili ulishaonekana?

12. Lwajabe aliporudishwa mara ya kwanza baada ya kutekwa, gari la Noah jeusi lilikuwa linazunguka mtaani kwake. Watu walilitilia shaka, wakachukua namba zake na kuwajulisha polisi. Mbona hadi sasa polisi hawajatoa taarifa juu ya hatua walizochukua dhidi ya gari hilo wala hawajasema ni la nani?

Bora Mambosasa angekaa kimya. Kama anatumwa aseme, awaeleza wanaomtuma kuwa wanaoelezwa kumsikiliza wana akili timamu, na wanachikozwa kusema mengine ambayo wasingeyasema iwapo asingesema.

Ndiyo, walimtisha Lwajabe asiseme wazi alichotendwa, lakini hakuna siri ya watu wawili.

Sawa, wafanye mizaha hii, lakini watambue kuwa damu ya Lwajabe ina thamani kama ilivyo damu ya Mambosasa. Tuheshimu utu wa wenzetu! Utu wetu ni bora kuliko vyeo na madaraka ya wanaomtuma kudhihaki uhai wa Lwajabe!

Imeandikwa na Ngurumo
 
Muhsini K Kwigwa

MAMBOSASA AMEIBUA MASWALI MAGUMU 12 KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Juzi niliandika kuwa Leopold Lwajabe, aliyekuwa Mkurugenzi wa miiradi ya Umoja wa Ulaya nchini (EU) katika Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye alikutwa ananinginia mwisho wa wiki, kabla ya kifo chake alilazimishwa kuandika wosia, wahusika wakauchomkea ofisini kwake kwa siri ili kuficha mazingira ya kifo chake.

Leo jioni nimemsikia Lazaro Mambosasa, Kamanda za Polisi Kanda ya Dar es Salaam, akithibitisha andiko langu kwa kulitokea maelezo, hasa kuhusu WOSIA. Mtu yeyote anayejua saikolojia, anaelewa kwanini Mambosasa amejitokeza kuzungumzia wosia huo.

Katika ndiko langu la awali lililosambaa kwenye mitandao ya kijamii nilisema:

INASIKITISHA: YA NDANI KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Dotto James, Katibu Mkuu Hazina (mpwa wa Raid Magufuli) ambaye ni bosi wa Leopold Lwajabe anatuhumiwa kuwa na mkono katika sakata la kifo cha LWAJABE.

Juzi kabla mwili haujapatikana Dotto alikuwa na vikao vya siri na polisi wasio na unifomu kujadili statement waliyopika kuhusu marehemu. Yeye alijulishwa kifo Jumamosi usiku, na Jumapili alishinda na hao polisi.

Lwajabe alikuwa akilalamika juu ya watu wanaomfuata kutaka hela za kitengo cha EU hapo wizarani. Alipokataa walimtisha kuwa wanamjua kila kitu na kuwa yeye ni raia wa Rwanda.

Katika kipindi hiki cha kuhangaishwa kwake, familia yake huko Karagwe ilihojiwa na maafisa usalama kuhusu uraia wake mara kadhaa.

Alipotekwa mara ya kwanza wiki moja iliyopita, alisainishwa makaratasi ya ofisi na kisha akalazimishwa kuwapa password ya ATM card na fedha zake zikachukuliwa zote.

Alirudushwa na gari la Noah na kutupwa jirani na kwake Kinyerezi. Waliomrudisha hawakutaka kujulikana. Gari jingine liliendelea kuzunguka eneo hilo kwa siku mbili kuchunguza kina nani wanafika na kutoka.

Yeye alikuwa kama amechanganyikiwa na akawa anatoa hadithi zinazojichanganya. Mwenyewe alitishwa kuwa akisema yaliyomtokea watarudi kummaliza. Wamemmaliza kimya kimya! Alipotekwa mara ya pili, wiki hii iliyoisha juzi, polisi waliendelea kuwatuliza ndugu zake kuwa ataonekana ndani ya saa 72, wakawaonya wasisemeseme sana.

Chanzo kutoka ofisi ya ZCO kinadai watekaji wake si polisi ila ni watu wenye nguvu waliokuwa wanawaagiza polisi mambo ya kufanya. Lwajabe alifanyiwa unyama mkubwa. Alilawitiwa na kupigwa picha. Alilazimishwa kuandika barua kuwa amejiua kwa sababu ya matatizo yake binafsi na kwamba asilaumiwe yeyote. Alilazimishwa kuandika wosia na ukapelekwa na kuingizwa ofisini kwake. Wauaji walimfunga kamba na kumtupa kichakani Mkuranga.

Kisha waliwaelekeza polisi waende kuchukua mwili na kuuweka hospitali. Polisi hawakwenda na camera kuchukua picha za eneo wala kuchukua alama za vidole mwilini. Mmoja wa wapelelezi ni ndugu ya marehemu, na alipogundulika polisi walisitisha jitihada zote za kupika ripoti. Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna kundi maalumu la siri serikalini lipo juu ya kila taasisi, na linachotaka ni fedha. Ni ujambazi wa kidola. Inasikitisha sana!

MASWALI YANAYOIBULIWA NA MAMBOSASA:

Kauli ya Mambosasa kuwa Lwajabe alijiua na aliandika wosia huo uliokutwa ofisini mwake, imethibitisha nilichoandika awali, na imeibua maswali mengine kadhaa.

Hapa naweka maswali 12 ya msingi ya haraka haraka ambayo Mambosasa angepaswa kuyajibu:

1. Mtu ambaye ameshaamua kujiua kwa kujinyonga mtini, hadi anaandika wosia na kuuacha ofisini, kwa nini atoke Dar es Salaam asafiri na kupita miti yote hadi Mkuranga, huku nyumbani kwake Kinyerezi kumejaa miti ya miembe ambayo ingemfaa kwa jambo hilo?

2. Lwajabe aliondoka nyumbani kwake akiwa amevaa shati. Amekutwa mortuary Mkuranga akiwa na tisheti. Kama Mambosasa ni mkweli, kwa nini hadi sasa dereva wake, karani wake na ndugu zake hawajahojiwa juu ya mabadiliko haya ya mavazi?

3. Kwanini polisi waliamua kumuondoa eneo la "kujinyongea" na kumpeleka mortuary bila kuita ndugu zake, wakati walikuwa na RB namba za kupotea kwake? Walikuwa na haraka ya nini?

4. Kwanini polisi hawakutumia forensic equipments ili kurahisisha uchunguzi?

5. Kwanini polisi hawakutaka ndugu wa marehemu kushiriki katika post-mortem na kwanini hawakuwapa taarifa za awali za uchunguzi?

6. Kwanini serikali ilijua wosia wa marehemu kabla ya kifo kutangazwa. Kwa nini polisi walikuwa wanamtafuta marehemu mezani kuliko vichakani?

7. Kabla ya kifo chake, kwanini maofisa usalama mkoani Kagera walisumbua familia yake na kuchukua maelezo yao baada ya Lwajabe kutekwa mara ya kwanza? Kwa nini mdogo wa marehemu aitwaye Meneja Byase alihojiwa na TISS kipindi marehemu ametekwa mara ya kwanza? Walihoji kuhusu nini, na mbona Mambosasa hasemi haya?

8. Kwanini Katibu Mkuu Hazina, Dotto James, alikuwa anamlazimisha Lwajabe aende likizo ya wiki mbili baada ya kuwa ametekwa mara ya kwanza?

9. Kwanini askari wa Kikosi Kazi (Task force) wasichukuliwe alama za vidole ili kulinganisha na alama za vidole kwenye baadhi ya vitu vilivyochukuliwa na askari aliyewatoroka na akaviacha kituo cha polisi Mburahati?

10. Kwanini polisi walikazana kutaka ndugu wa marehemu wasisemeseme na kwamba ndugu yao angeonekana ndani ya saa 72 baada ya kutekwa? Walijuaje? Lengo lao lilikuwa nini?

11. Kwanini Katibu Mkuu Dotto alizuia kifo cha Lwajabe kutangazwa Jumamosi jioni wakati mwili ulishaonekana?

12. Lwajabe aliporudishwa mara ya kwanza baada ya kutekwa, gari la Noah jeusi lilikuwa linazunguka mtaani kwake. Watu walilitilia shaka, wakachukua namba zake na kuwajulisha polisi. Mbona hadi sasa polisi hawajatoa taarifa juu ya hatua walizochukua dhidi ya gari hilo wala hawajasema ni la nani?

Bora Mambosasa angekaa kimya. Kama anatumwa aseme, awaeleza wanaomtuma kuwa wanaoelezwa kumsikiliza wana akili timamu, na wanachikozwa kusema mengine ambayo wasingeyasema iwapo asingesema.

Ndiyo, walimtisha Lwajabe asiseme wazi alichotendwa, lakini hakuna siri ya watu wawili.

Sawa, wafanye mizaha hii, lakini watambue kuwa damu ya Lwajabe ina thamani kama ilivyo damu ya Mambosasa. Tuheshimu utu wa wenzetu! Utu wetu ni bora kuliko vyeo na madaraka ya wanaomtuma kudhihaki uhai wa Lwajabe!
Nimesoma kwa kuogopa sana... Tena sana.... The fear is real.....
 
Back
Top Bottom