Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Kama kuna kitu wanachokisubiri na kukingojea Watanzania walio wengi basi ni anguko la CCM litakalopelekea kifo chake,vingi ya vyama vilivyopigania uhuru wa Nchi zao sasa vimebakia kama ni historia .
Matarajio ambayo huenda yakaanza kuonesha dalili za kifo cha CCM ni uchaguzi mkuu hapo mwezi wa kumi,masikio ya WaTz kwa sasa yameanza kugeukia mwezi huo na kujiandaa kusikia kuwa CCM imeaga Tanzania kama si dunia.
Aminia siku hizi kuonekana wewe mwananchi wa kawaida ni ccm imekuwa noma sana ,baadhi huwa wanajitokeza siku za sherehe za ccm na makongamano yao ndio utawaona wakivaa sare za kiccm ,tofauti na kuta wananchi wa vyama vingine ambao huvaa sare za vyama vyao bila hata ya kuwepo na dalili za mkutano na imekuwa kawaida kutembea nazo ,ila kwa wanaojiita wanaccm ni mtihani mkubwa kuivaa sare na kutembea nayo ,hiyo ni dalili tosha kuwa chama kimepoteza mvuto na imekuwa ni chama aibu.