Kifo cha CCM Bukoba mjini

Kifo cha CCM Bukoba mjini

Omulangira

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
230
Reaction score
29
Wapendwa wanaharakati CHADEMA kupitia mpango wake wa M4C imeendelea kukizika Chama cha Mapinduzi katika manispaa ya Bukoba baada ya kufanikiwa kumpata mwanachama mpya Mkazi wa Hamugembe ajulikanaye kwa jina la Mzamilu Abdul Kamalitie katika mkutano wa Hadhala uliofanyika jana kwenye viwanja vya Hamugembe ukiongozwa na Kamanda Alphonce Mawazo aliyesaidiana na makamanda wengine ambao ni Husna kutoka Buseresere na kamanda mpya aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya mkoa kupitia CCM willayani Muleba Bwana Hamis Gaga.

Kamalitie hakuwa na cheo chochote ndani ya CCM lakini alikuwa ni mpiga debe mzuri kwani ndiye aliyekuwa akitumika kama MC kwenye mikutano yote ya CCM. Kwa umaarufu wake Kamalitie amewahi kuwa Swaiba wa mbunge wa sasa wa Bukoba mjini kiasi cha kumpa kaziu katika redio yake ijulikanayo kama Kasibante.

Kwa maelezo zaidi fuatilia matukio katika picha
 

Attachments

  • DSC03449.JPG
    DSC03449.JPG
    1,011.5 KB · Views: 314
  • DSC03452.JPG
    DSC03452.JPG
    1.1 MB · Views: 451
  • DSC03454.JPG
    DSC03454.JPG
    1.2 MB · Views: 248
  • DSC03456.JPG
    DSC03456.JPG
    857.8 KB · Views: 191
  • DSC03458.JPG
    DSC03458.JPG
    745.9 KB · Views: 186
  • DSC03460.JPG
    DSC03460.JPG
    787 KB · Views: 166
  • DSC03482.JPG
    DSC03482.JPG
    248 KB · Views: 126
  • DSC03480.JPG
    DSC03480.JPG
    706.5 KB · Views: 139
  • DSC03461.JPG
    DSC03461.JPG
    599 KB · Views: 142
  • DSC03462.JPG
    DSC03462.JPG
    807.3 KB · Views: 95
  • DSC03471.JPG
    DSC03471.JPG
    811.5 KB · Views: 135
good news waizike kabisa ccm tumechoka nayo hakuna inachofanya chakujivunia; elimu chini, afya mahututi, kilimo mwisho, maji salama ni kilio cha kila siku, nyumba bora kwa mlalahoi ni ndoto za mchana, tunahitaji changes na uponyaji wa taifa letu
 
Ndugu zangu miaka yote huwa wananiangusha sana, lakini sasa hivi nahisi wameanza kuamka na kuona mwanga angavu wa jua uashiriao WAKATI WA MABADILIKO NI SASA, pia naamini wameshaanza kutambua ya kuwa na wao wananafasi na wajibu wa kuleta mabidiliko ya kweli yaliyo chanya kwa mustakabali wa Taifa letu sasa na vizazi vijavyo!
HONGERENI SANA, TUSIMAME IMARA MPAKA KIELEWEKE!
 
wakaze buti, wananchi wa kanda hii wameamka sana
 
Harakati hizo ziendelee nchi nzima kwani tumesha wachoka ccm ila nawasihi, harakati hizo ziendelee mpaka 2015
 
Wana-CCM acheni kurandaranda mijini na kuruka mi-pipa kutafuna pizza katika nchi za watu Ughaibuni, e nendeni mkaokoe chama chenu kule kwa wananchi vijijini.
 
Kazi ni moja tu kuuwa ccm kama tupigavyo kichwa cha nyoka
 
Kazi nzuri kamanda Mawazo, umepata mwanachama mmoja wa CCM angalau, yule hawala anayegaramiwa safari zake na chama na posho za madereva na wapambe wake huwa hana anachopata zaidi ya kuongeza migogoro tu.
 
Wapendwa wanaharakati CHADEMA kupitia mpango wake wa M4C imeendelea kukizika Chama cha Mapinduzi katika manispaa ya Bukoba baada ya kufanikiwa kumpata mwanachama mpya Mkazi wa Hamugembe ajulikanaye kwa jina la Mzamilu Abdul Kamalitie katika mkutano wa Hadhala uliofanyika jana kwenye viwanja vya Hamugembe ukiongozwa na Kamanda Alphonce Mawazo aliyesaidiana na makamanda wengine ambao ni Husna kutoka Buseresere na kamanda mpya aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya mkoa kupitia CCM willayani Muleba Bwana Hamis Gaga.

Kamalitie hakuwa na cheo chochote ndani ya CCM lakini alikuwa ni mpiga debe mzuri kwani ndiye aliyekuwa akitumika kama MC kwenye mikutano yote ya CCM. Kwa umaarufu wake Kamalitie amewahi kuwa Swaiba wa mbunge wa sasa wa Bukoba mjini kiasi cha kumpa kaziu katika redio yake ijulikanayo kama Kasibante.

Kwa maelezo zaidi fuatilia matukio katika picha
CCM ITAKUFA KWA SABABU HII…….

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.


Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?


Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA?

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa???
 


.....inapendeza sana kuwaona hapo juu mama zetu wame chachamaa kuyazika magamba!!!


wana maanisha:


"..kanga na kofia vaeni wenyewe...we need education for our children "
 
Pengine unaweza kutokubali huu ushauri.
mimi nipo hapa bk kwa muda mrefu sana lakini siasa za CDM,CCM na CUF hapa nafikiri hazina mashiko sana.Ni siasa za kutafuta fedha kwa walio wengi.watu wanatafuta maisha kupitia siasa badala ya kufanya kazi/kuwajibika.

Wafanya siasa wengi hapa ni wajasiriamali wa siasa.

Mfano ukifika kwenye matawi,mashina nk hakuna hamasa kuhusu vyama bali wanasubiri mpaka viongozi kutoka mikoa ili wafike bk kufanya mikutano ya hamasa na kuimarisha vyama vyao.

Nasema hivi kwa kujiamini,natumia jina langu halisi nk.Tufike hatua tuelezane ukweli
 
Wapendwa wanaharakati CHADEMA kupitia mpango wake wa M4C imeendelea kukizika Chama cha Mapinduzi katika manispaa ya Bukoba baada ya kufanikiwa kumpata mwanachama mpya Mkazi wa Hamugembe ajulikanaye kwa jina la Mzamilu Abdul Kamalitie katika mkutano wa Hadhala uliofanyika jana kwenye viwanja vya Hamugembe ukiongozwa na Kamanda Alphonce Mawazo aliyesaidiana na makamanda wengine ambao ni Husna kutoka Buseresere na kamanda mpya aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya mkoa kupitia CCM willayani Muleba Bwana Hamis Gaga.

Kamalitie hakuwa na cheo chochote ndani ya CCM lakini alikuwa ni mpiga debe mzuri kwani ndiye aliyekuwa akitumika kama MC kwenye mikutano yote ya CCM. Kwa umaarufu wake Kamalitie amewahi kuwa Swaiba wa mbunge wa sasa wa Bukoba mjini kiasi cha kumpa kaziu katika redio yake ijulikanayo kama Kasibante.

Kwa maelezo zaidi fuatilia matukio katika picha

PICHA ZINAONYESHA KANA KWAMBA NI KAKIKAO KA MSIBA VILE.

Hapana hapa nakukatalia huyu jamaa ni kibaka tu wa mtaani hana influence yoyote na hana madhara kwa CCM kwani naye hanazo njaa za wana bukoba za tumbo na kichwa!!!!!!
 
Tunaomba kamanda Alphonce Mawazo na wenzake wafike hadi vijiji vya huku mikoa ya Lindi na Mtwara.
 
M4C iwe vijijini tuu kwa sasa.TAFADHALI VIONGOZI ZINGATIENI HILI
 
Cjui km unamfahamu vizuri huyu bwana alikuwa na inluence hasa wakati wa mikutano hadhara alikuwa anatumika km MC
 
si mbaya ila bado nakuuliza kamanda Mawazo,mbona sioni mikutano kemondo,maruku,katerero,lyamahoro? mbona hamhami maeneo?
 
Harakati hizo ziendelee nchi nzima kwani tumesha wachoka ccm ila nawasihi, harakati hizo ziendelee mpaka 2015.

.......

Mbona wenyewe yanawashinda?wangapi wametoka CHA-DEMOLITION kwenda SISIM.
 
Asante sana Omulangila...........Kazi iendelee. Usisahau leo Kikao saa 10 jioni kwa ajili ya kumalizia Strategic Plan ya CDM kwa Bukoba na baadae KAgera yote. Karagwe wameshamaliza tayari CCM hakuna kule. Niko njiani natokea Biharamulo.
 
kutafuta fedha kwa walio wengi.watu wanatafuta maisha kupitia siasa badala ya kufanya kazi/kuwajibika. Kwa kiasi fulani uko sahihi maana wahaya kwa kawaida ni ndumilakuwili hivyo si ajabu kuwa na tabia kama unazozisema. Ila kwa ninvyowajua akina nshomile hawawezi kuwa tayari kuzidiwa na watu wa Mtwara katika swala zima la kujitambua, siamini kwamba pamoja na undumilakuwili wao kama wamefurahishwa na division Zero nyingi za form IV kwa watoto wao lakini la zaidi ni huu mgogoro mkubwa unaoendelea kati ya wanaCCM wenyewe ( Kagasheki na Diwani). Uwezo wa kutambua wanao na hivyo bila shaka ufumbuzi ni kukipiga mweleka CCM katika uchaguzi ujao. Siasa haziwezi kunoga kama hakuna makubwa yoyote yalifanywa au mabaya yaliyofanywa na chama kikichopo madarakani. Mazuri ni mtaji kwa CCM wakati huo huo mabaya ya CCM ndo mtaji wa upinzani, Chadema wanao mtaji wa mabaya inayoendelea kuyafanya CCM usilisahau hilo lakini pia kwa Bukoba mjini si mara ya kwanza kwa upinzani kuwa na wapenzi wengi kuliko CCM
 
Back
Top Bottom