Kifaa cha kudhibiti matumizi ya fedha chazinduliwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,267
Kampuni moja ya uingereza inatarajia kuweka kifaa kinachodhibiti matumizi ya fedha kwa kuwapatia wateja wake mshtuko wa umeme iwapo atapitisha kiwango cha matumizi yao.
Kampuni ya Intelligent Environments, imezindua mfumo ambao utaiunganisha na mpira wa kuvaliwa mkononi wa pavlok ambao unatoa mshtuko wa volti 255 kwa akaunti ya benki, iwapo fedha katika akaunti zitashuka kupita kiwango mteja alichokubali.
Mtendaji mkuu wa kampuni ya Intelligent Environments, David Webber alisema wazo hilo lilikuwa kuhusu pendekezo la wateja.
Hakuna benki yoyote imetangaza itaanzisha mfumo huo kwa wateja, lakini benki hiyo ya mtandao wa Intelligent Environments imetaja benki kadhaa za uingereza kama wateja wao wanaotumia mifumo yake ya mtandao.

ba41b3d80e49dae3cf52a9dfc2c26d6b.jpg
 
Back
Top Bottom