Kidono/Vidono

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,125
1,752
Habari za humu ndani wakuu, Naomba kujuzwa kwa ukweli wa Kidono au Vidono.... "hapo zamani nimekuwa nikisikia huyu kachanjiwa vidono hawezi kufa kirahisi" hasa kwa wezi au majambazi.

Kidono huchanjwa watu kama kinga ili kujikinga wasidhurike, tu akichomwa kisu hafi au akipigwa bunduki haimdhuru hii imewapa tabu sana watu wa usalama enzi hizo.

Kidono kwa nilivokuwa nasikia asiri yake ni Kigoma na wakati mwingine watu hujichanja kama utamaduni, mtu aliejichanja Kidono hata ukipigana nae lazima utoke nduki, kwa wale wezi wanaposhikwa nilikuwa nikisikia mpaka wamkate na upande wa kisu ambao ni butu ndo ana dhurika na siri ya kidono hujua mke au familia ya muhusika aliejichanja wengine watu wa Pembeni hamuwezi kujua.

Watu waliojichanja Kidono huwa watemi/wababe sana kuna mmoja ilifikia hatua Porisi wamekuja kumshika kwake Gari la Porisi halikuweza kuondoka eneo lile mpaka Baba yake mzazi mttuhumiwa alipomuomba "Baba wasamehe we nenda kawasikilize tu" ndipo Gari liliweza kuondoka.

Kidono ni maarufu maeneo ya Tabora na Kigoma

KIDONO Mwnye kufahamu zaidi atutupie madini.
 
Yaah...Vidono ni utamaduni wa kuchanjia asili yake Buha-Kigoma. Ila kabla unatestiwa kama imekolea kwa kukatwa panga likidunda basi...lakini kama bado ndo nitolee.
Mtu huyo anaweza hata kupigana na watu 20 na wakafloat,risasi inadunda,kisu,panga ,mshale havifui dafu.
 
hahahahhaha kwahiyo wakikutest ukikatwa ujue bado..? vipi kuhusu wale ambao wanafukiwa Kaburini siku7 then wanafukuliwa au kuwekwa kwenye pipa la maji ya moto kama kipimo chakuzindikwa ili wakomae vizuri..?
 
Nadhani hapa kwenye kipimo kama dawa imefana ndipo kwenye ugumu wa hii chanjo.
 
hahahahhaha kwahiyo wakikutest ukikatwa ujue bado..? vipi kuhusu wale ambao wanafukiwa Kaburini siku7 then wanafukuliwa au kuwekwa kwenye pipa la maji ya moto kama kipimo chakuzindikwa ili wakomae vizuri..?
Eh hii sasa kali kufukiwa siku saba?? Hapana kwa kweli
 
Kuna jirani yetu mmoja zamani nikiwa mdogo ....cha pombe balaa umri umeenda kidogo(mtu wa makamo).Sasa kuna kijana mmoja alinunua kiwanja mtaani kwetu akajenga mjengo wa maana.!Huyu jamaa alikuwa full nyodo alafu jeuri,mbabe dizain jitu la miraba minne.

Sasa siku moja(usiku kama saa sita-saba) yule mzee alikuwa anatoka kilabuni kautundika....anapandisha nyumbani,anapita jirani na nyumba ya jamaa ,anaimba nyimbo za kilevi.....

Jamaa katoka nje ana mfokea'we mlevi acha kelele zako" na matusi juu...mzee kakasirika! "kwanini unanitukana nimekukosea nini??
Jamaa kwaku jua mlevi akakata fimbo amcharaze ili pombe zimuishe!! wee...jamaa alipewa vitasa balaa (maana ngumi jiwe) akazimia hoi...akakimbizwa hospitali taharuki mlevi kamfloatisha kijana mtu wa miraba minne!! Ndio tukaja kuambiwa mzee huyu wa kiha /kigoma alichanjiwa Vidono!!
 
Back
Top Bottom