Kidole changu kimepona asanteni JamiiForums

Kipesani ni lugha za huo mkoa wa kusini wanaopenda wanawake kuliko pesa sio kiswahili hicho

Mkuu ndula ni kilugha au maana kiswahli inaitwa ndulele


....inaitwa tura bwana na sio ndula

Wakuu, majina yote hayo ni sawa.Kiswahili ni mchanganyiko wa maneno toka lugha nyingi za makabila yetu, na Lugha nyingi za kigeni kama kijerumani,kiingereza,kiarabu, kipersia, kireno, na hata kifaransa.
 
Tatizo mnaandika majina yenu ya asili na hivyo sii rahisi watu wengine kujua ni kitu gani......Jina la huo mmea ni "NDULELE"
 
Nafikili mdudu huyo chakula chake ni ndula ndo mana katoka haraka kufakamia ndula
 
Hongera kwa kuleta mrejesho. JF ni shule ya aina yake.

Kuna kipindi hapo nyuma wiki iliyopita nliweka post hapa kuhusu kidole changu kilichovimba ikidaiwa kina mdudu ndani, Nilienda hospitalini waliniambia nitumie dawa za ammoxylin na panadol lakini hazikusaidia, Nikabadilisha hospitali nikaenda nyingine wakaniambia nitoe kucha nikaona ngoja nitumie ushauri niliopewa na wana jf wa kutumia Ndula, Hio ndula niliichuma nikaikata juuu na chini na kuipachika sehemu iliyovimba kama vile pete. Nliivaa kwa siku mbili na kidole kimepona kabisaaaa...

SHUKRANI SANA WANAJAMII FORUMS
 
Kwahiyo mkuu ulivaa kama pete kwa siku ngapi ukitaka kuoga ulikuwa unavua hiyo pete ama?
unaivaa kwa masaa 24 ,mimi nlivaa kwa siku mbili kwa jumla ya masaa 22 hivi mana kuna sehem nyingine nlikuwa navua na nikienda kuoga naivua jata nikiwa kwenye mzunguko navua ila nikifika home ama wakati wa kulala naivaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom