Katibu Mkuu Ardhi aingia matatani
Posted on by UHURUPUBLICATIONS
NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa zamani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,ambaye kwa sasa ndiye mkuu TRA bwana Alphayo Kidata, aliingia matatani kutokana na kudaiwa kujiuzia gari aina ya Toyota Land Cruiser.
Gazeti hili lilibaini kuwa kigogo huyo amejiuzia gari hilo kwa bei ya chini ya sh. milioni tano ikiwa ni kipindi kifupi baada ya kufanyiwa matengenezo yaliyogharimuzaidi ya sh. milioni 55.
Habari zilidai kabla ya kuuzwa gari hilo lilikuwa likitumiwa na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Akiwa madarakani, Profesa Tibaijuka aliwahi kupata ajali na gari hilo, Toyota Land Cruiser VX V8, maeneo ya Kahama mkoani Shinyanga.
Gari hilo lililokuwa na namba STK 5857, lilikuwa likitokaBukoba kwenda Dodoma na katika ajali hiyo si Profesa Tibaijuka wala dereva wake aliyeumia. Ajali hiyo ilitokea baada ya kugonga punda.
Uamuzi wa Kidata kujiuzia gari hilo maarufu kama shangingi, kimelalamikiwa na baadhi ya watu kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.
Ilielezwa kuwa kitendo cha kiongozi huyo kujiuzia gari kwa bei nafuu baada ya kulifanyia matengenezo kwa gharamakubwa tena ikiwa ni fedha za serikali, kinatoa picha mbaya kuhusiana na dhamira yake ya matumizi ya fedha za umma.
Ilielezwa kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za manunuzi ya vifaa chakavu serikalini, ilipaswa jambo hilo litangazwe hadharani ili kuwe na ushindani wa bei.
Habari zaidi zilifafanua kuwa hata kama gari hilo litakuwa limelipiwa kodi baada ya kuuzwa kiasi kinachoweza kutozwa si zaidi ya sh. milion16, hivyo kufanya jumla kuwa takribani sh. milioni 20.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Kidata alishindwa kulizungumzia baada ya kusema aliitwa kwenye Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu Mtaa wa Lumbumba, Dar es Salaam. “Nipo Lumumba (CCM) kwa sasa nimeitwa,” alisema kwa ufupi Kidata na kukata simu na alipopigiwa mara kadhaa baadaye simu yake ilikuwa inaita bila kupokea.