Kichwa kuuma juu ya jicho

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Wasalaam wadau wa afya.

Hivi ninavuoandika uzi huu kichwa kinaniuma upande wa juu ya jicho la kushoto zaidi ya saa moja sasa.

Siku ya leo sijatoka ndani, nimepumzika Karibu siku nzima, nimekunywa maji ya kutosha pia.
Nimesoma soma email tu na Internet kidogo.
Hali hii ishawahi kunitokea tena siku za nyuma, huwa najitahidi sana kuepuka dawa, inapotokea hivyo nakunywa tu maji na kuoga maji ya kawaida.
Leo nimefanya hayo bila mafanikio imebidi nimeze panadol mbili muda huu, lakini maumivu bado yapo.

Sasa naomba kufahamu hivi hii yaweza kuwa tatizo gani? Au dalili za tatizo gani?

Ushauri kwa ambaye kashakutana na hali hii, Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom