Kibwagizo cha "HAPA KAZI" na mvinyo wa maisha bora kwa mtanzania

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,291
Kama move vile inaendelea. Episode imekwisha ya nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya na ile ya maisha bora kwa kila mtanzania.

Sasa ni episisode namba 2. "Hapa kazi tu" watanzania wanaendelea na maisha yao kwa sasa tunaona uhalisia kuwa mzunguko wa fedha umekuwa hafifu mikononi mwa wananchi. Vitu vimepanda bei maradufu na manunguniko ya vijana kukosa kazi.

Vyombo vya habari ni kama vimekumbwa na mvinyo wa hapa kazi tu. Vinaserereka na mdundo vinasifu kutumbuwa majipu vimeacha kuibua njia za kuzuiya majipu yasiote.

Bahati mbaya mvinyo wa mara hii umekuja na nguvu sana unafoka kwa presha. Prewsha hii ya mzuka imewapumbaza wengi. wamesahau kwamba hili ni povu tu chupa ni ile ile.

Zamani ikiitwa Maisha bora kwa kila mtanzania sasa inaitwa HAPA KAZI TU.

Tusiache ajenda watanzania wanataka mabadiliko ya kweli.
 
Back
Top Bottom