Kiburi ni kizuizi cha Neema ya Mungu kwa Mtu

Kiburi ni kizuizi cha Neema ya Mungu kwa Mtu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Yer 48:29 SUV
[29] Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake.

Moabu lilikuwa ni taifa lililojitukuza yenyewe, lilijiona lenye nguvu na fahari nyingi, likaacha kumtegemea Mungu na kujitegemea lenyewe.

Ukiangalia katika agano la kale utaona baadhi ya hukumu zilisababishwa na kiburi, na ukija katika agano jipya napo dhambi ya kiburi imeelezwa, ambapo inahusishwa na hali ya moyo ulioinuka na kuikataa neema ya Mungu.

Ukiangalia kiburi cha Moabu, utaona kikipingana na mfano wa Kristo wa unyenyekevu, na Mungu huwapinga wale wenye kiburi. Lakini cha kushangaza huwapa wanyenyekevu neema.

Yakobo 4
6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

Neema hii aliikosa Moabu, sababu aliyomfanya aikose hii neema ni kule kujikutukuza kwake, kule kujiona kila kitu anakiweza, kule kuona nguvu zake zinamtosha na kuacha kutafuta msaada wa ki-Mungu, na kufuata vile anataka.

Moabu alifika hatua kujiona yeye ni shujaa, kama ambavyo siku za leo mtu anaweza kujiona ana uwezo mkubwa wa kufanya lolote hapa duniani. Pamoja na Moabu kujiona shujaa, hakujua janga lililokuwa karibu yake kumtokea.

Ndivyo na kwetu leo, mtu anaweza kukosa kuona hatari iliopo mbele yake, na hitaji lake kutoka kwa Mungu kutokana na kiburi chake, kwa sababu kiburi kinazuia kuona hitaji la msingi.

Ufunuo 3
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Mtu mwenye kiburi hana toba, mtu asiye na toba hana unyenyekevu, na ukikosa unyenyekevu huwezi kupokea mabadiliko ya kweli kutoka kwa Mungu.

Ukiangalia mfano wa mtoza ushuru katika Luka 18:9-14 utaona vile unasisitiza jinsi Mungu anavyoweza kuwakubali wale waliovunjika moyo kwake.

Mtu anayekataa kutubu ana kiburi, mtu huyo hana Yesu moyoni mwake, ni mtu anayejitemea yeye, anajivunia nguvu zake, mambo ya wokovu kwake sio hitaji la msingi.

Andiko la msingi la Yeremia 48:29 nililoanza nalo hapo juu, linatoa onyo dhidi ya roho ya kujitukuza, linaonyesha vile mtu anaweza kuinuka katika huduma, uongozi, au mafanikio ya kiroho au kimwili na asiitambue nafasi ya Mungu katika maisha yake.

Napenda uelewe kuwa kiburi chochote huzaa anguko baya kwa mwenye kiburi, madhara yake ni makubwa kuliko tunavyoweza kueleza hapa.

Mithali 16
18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

Angalia mfano wa Yesu, alikuwa mnyenyekevu sana, ukiona mambo yako mengi hayafanani na Kristo, nikimaanisha tabia yako na mwenendo wako, ujue umepishana naye mbali.

Kila huduma au karama kuna neema ya Mungu juu yake, hicho unachokifanya bila neema ya Mungu kuwa juu yako hutokiweza, uongozi, au utumishi wako unahitaji kufunikwa na neema ya Mungu. Sasa ukiingiwa na kiburi hiyo neema huondoka na kukaa mbali nawe.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom