Kibu Denis: Diarra angedaka ule mshale wangu hadi sasa angekua anajiuguza kwao Mali

Huyu huwa namwonea huruma, ni mpambanaji, anatafuta ugali kama wengine tu, ila mpira hajui, anajua tu kukimbiakimbia, hatumii akili. hata hivyo watu kama hao wanahitajika kwenye timu na wana faida kwa upande wao, waendelee tu kumweka kwenye timu na ni mhimu kumsaidia kimaisha. nimejitahidi kutoa fair comment.
Mkuu, Kwa wazawa kibu denis ni moja ya wachezaji bora sana. Tanzania tunawachezaji bora wachache sana.

Ukitaka kujua Kibu ni bora, angalia strength za kibu kama Kibu.
Hakuna Coach atakuja pale Simba akamkataa Kibu D, labda awe Kocha mzawa sababu anasikiliza maneno ya mtaa.
 
Tukiwa tunaelekea kwenye maadhimisho ya wana-lunyasi "Simba Day 2023" basi matukio na hisia tofauti zimeanza kuipamba siku hiyo.

Kati moja ya matukio hayo, basi ni yale aliyoya-eleza Kibu D, anaenda kwa jina la "Kibu Mkandaji", jina ambalo lilipata umaarufu baada ya kuwakanda Wananchi April 16, 2023.

Anasema:

" .....Ni kweli nilikua na nafasi ya kutoa pasi kwa mchezaji mwenzangu, ila nikai-ambia akili yangu hapa napiga, hapa nalenga lango, basi na kweli mpira ukakubali nikatuma kombora, ila ndugu yangu(Mdaka mishale) alijaribu ila waaapi?

Akaendelea kusema;

Angethubutu(angaleta kiherehere) cha kudaka, basi hadi sasa angekua kwao Mali anajiuguza maana ule mshale ulikua wa moto sana".

Mwisho amewakaribisha watanzania kujitokeza katika Tamasha la Simba huku akichagiza kuwa huko Uturuki anaona watu waona wachezaji wa Simba wenye U-Messi, Messi. Pia, Watanzanzia wajiandae na pira "Uturuki".

(Nime-attach video yake pia)

Huyu nae kubebwa na kocha tu ndege kumnyea mtu si shabaha
 
Back
Top Bottom