Kibonoka genius

mickey drizzy

Member
Joined
Jun 19, 2015
Posts
30
Reaction score
3
Wazee wawili walikua wamekaa chini ya mti wakizungumza kuhusu watoto wao huku kila mtu akimsifia mtoto wake:

BABA KIBONOKA: Wewe huniambii kitu, mwanangu ana akili kuliko hata wako
BABA KIPONDO: Mwanao zero tu hana kitu
BABA KIBONOKA: Aaah! wewe humjui yule, hapa kwenyewe yupo ndani anajisomea
BABA KIPONDO: Aaah wapi.. labda sio Kibonoka ninaemjua mimi.. aache kucheza asome? mwenzake Kipondo yuko ndan anasoma
BABA KIBONOKA: Acha kuzuga wewe muite wako na mimi nimuite wangu
BABA KIPONDO: We KIPONDO
KIPONDO : Naam
BABA KIPONDO : Njoo na ulichokua unakifanya

Mara akatoka Kipondo akiwa amebeba madaftari yake
KIPONDO : Hii hapa baba
BABA KIPONDO: Baba Kibonoka umeona? haya muite wako

BABA KIBONOKA HUKU AKIJIAMINI: We "KIBONOKA"
kimya
We "KIBONOKA" si nakuita huniskii au dharau hebu njoo na hayo madaftari yako

KIBONOKA AKAITIKA AKIWA JUU YA ULE MTI: Daaaah! Mzee kausha kwanza nimtoe huyu ndege maana nimetega tangu juzi asubuhi hata shule sijaenda...

Kama wewe ndo baba, ungefanyaje?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…