Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Polisi nchini imesema ifikapo Desemba 31 kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe zimejisajili na kuwasajili walinzi wake kwenye mfumo wa uboreshaji wa sekta ya ulinzi binafsi kwa njia ya kielektroniki (PSG-P).
Kampuni ambazo zitashindwa kutatekeleza agizo hilo hazitaruhusiwa kufanya kazi nchini.
Akizungumza hivi karibuni kwenye kipindi cha Kumekucha kinachorushwa na kituo cha ITV, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Narcis Missama alisema mfumo huo unajumuisha kanzidata itakayokuwa na taarifa zote muhimu za kampuni binafsi za ulinzi.
Missama alisema kanzidata hiyo itakuwa na taarifa za vibali halali vya kufanya kazi za ulinzi nchini, wafanyakazi wa kila kampuni na taarifa zingine za wadau muhimu wa sekta hiyo.
Alisema usajili wa kampuni na wafanyakazi wake inaendelea na kwamba lengo la mfumo huo ni kuboresha sekta ya ulinzi ikiwamo kuhakikisha kuwa kila mlinzi anakuwa na sifa stahiki na amepata mafunzo yatakayoratibiwa au kutambuliwa na Polisi.
Pia, alisema PSG-P unaotekelezwa kwa pamoja na vyama vya kisekta; TSIA na Tamasca chini ya usimamizi wa Polisi, utarahisisha upatikanaji taarifa za mlinzi kwani kila mmoja atakuwa na kitambulisho chenye namba maalumu inayotolewa na Polisi.
Alisema baada ya usajili kila mfanyakazi atapewa kitambulisho chenye ‘QR Code’ hivyo kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta anaweza ku-scan na kuziona taarifa zote muhimu za mlinzi husika mara moja hivyo, kuwezesha utambuzi wao haraka.
Kuhusu faida ya mfumo huo, Missama alisema licha ya faida za usalama kwa mtumia huduma, itasaidia kukuza uchumi kwa kuwavutia zaidi wawekezaji kwani watakuwa na uhakika wa kupata huduma za ulinzi zenye viwango.
Akitoa historia fupi ya sekta hiyo, alisema sekta ya ulinzi binafsi nchini imekuwa kwa kiwango kikubwa kuanzia miaka ya 1980 baada ya kuruhusiwa ikiwa na kampuni tatu.
Chanzo: Mwananchi