Kibaha Mjini: Mh. Koka awafunda bodaboda kutojihusisha na maandamano

mwanakidagu

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
208
78
MH. KOKA,Mbunge wa jimbo la kibaha Mjini ,amefanya kikao na waendesha pikipiki ali maarufu bodaboda jana.

Koka akiongozana na uongozi wa juu wa wilaya,akiwa na mkuu wa wilaya bi .Halima Kihemba-,na bi .Tatu, Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mjini kwa nafasi zao waliwafunda bodaboda kwa mambo yafuatayo;
  1. Kujiepusha na maandamano ya vyama vya siasa
  2. Kulipa kodi
  3. ahadi ya kumiliki bodaboda zao
  4. kujikinga na ajali za barabaani
YEYE KOKA alijikita na ahadi namba moja ya maandamano na kutojihusisha na masula ya ushabiki wa kisiasa,;vyama vya siasa vina wavuruga kwa kuwatumia katika maandamano yao ,jiepusheni na maandamano hayo fanyeni kazi zenu mjipatie vipato halali,bila kutaja chama,lakini niani mwake kwa mtu anayetambua alikilenga chama kikuu cha ushindani na ccm CHADEMA,kuwa ndicho chama kina lalamikiwa kuendesha maandamano .

UKWELI WA MAMBO hapa kibaha mjini unatokana na kasi ya CHADEMA kufungua matawi ya msingi viungani mwa mji hivyo kumemfanya Koka kuwa na hofu na kibarua chake kilichotokana na kupewa kura na wananchi hapo 2010.Huku akiungana na mkurugenzi wa mji bi Tatu,wamekipa muda wa wiki moja CHADEMA kubomoa matawi msingi yao ya mail moja,soko kuu na la tatu lilipo kuwa soko la kila jumamosi.

Kiongozi wa juu wa CHADEMA alihoji uhalali wa mkurugenzi kuendelea kuwabeba ccm ambao matawi yao yapo karibu na yale ya CHADEMA ,amesema yetu tuyavunje ndani ya wiki moja,je na ya ccm itakuwaje kwa maana sote tumejenga maeneo yale yale.

Sisi Kama CHAMA KATU HATUWEZI KUYAVUNJA ILA TUNANGOJA HATUA ZAIDI TOKA KWAO,KAMA TUMEVUNJA SHERIA TUKUTANE MAHAKAMANI,KWANI SISI TUNA WAKILI WETU PROFESA SAFARI NA NDIYE MLEZI WA KANDA YETU.

Pia katika kikao hicho aliwataka bodaboda kulipa kodi TRA,Kama ambavyo wanapaswa ili kuwa na uhalali wa kufanya kazi zao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kibaha mjini aliwaasa boda boda kukaa mbali na pilika pilika za kisiasa,na maandamano badala yake wafanye kazi zao pia aliwaomba wajiandikishe majina yao ili atafute uwezekanao wa kuwapatia pikipiki kila mmoja ili wazimiliki tofauti na hivi sasa ambapo wanafanyia kazi mabosi wao waliowaajiri.pia aliwaasa kufuata sheria za barabara ili kuepuka ajali.
 
Back
Top Bottom