Kiapo wanachoapishwa viongozi huwa ni vitabu vya dini kweli?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Wakuu,

Poleni na pilikapilika na harakati za kutafuta chochote kitu ili mikono iweze kupishana kinywani kwa kawaida hua tunaona viongozi mbalimbali wakiapishwa kwa kulingana na sheria zetu zinavyosema lakini kwa mujibu wa vitabu vyetu vya imani huwa tunaona wakati anapishwa kiongozi hushika anashika kile kitabu anakinyooshea juu anaapa,sasa hapa huwa najiuliza hivi hua vinakuwa ni vitabu au ni majalada tuu wakuu maana sijawahi ona wakitoa mstari hata mmoja mle ndani wakampa muapishwaji akajisomee mbele ya safari.

Nawasilisha naomba kujuzwa hivi ni vitabu kweli?
 
Nasita na viapo wanavyoapa binafsi ningelipenda vifutwe maana viapo vyao naona kama ndiyo vyanzo vya matatizo yanayotupata kwa sababu kuna kumchezea Mwenyezi Mungu matokeo yake nchi inashushiwa laana ajali kibao kuchinjana usiseme ujambazi hauishi na mengi yanayotokea nchini kwa sababu hakuna ayekula kiapo cha kuyatekeleza yanayopaswa kutekelezwa.
 
Back
Top Bottom