Khutba kuhusu kuwa na uhakika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Khutba kuhusu kuwa na uhakika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Jun 18, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Moja ya khutba kubwa aliyohubiri Yesu katika hekalu wakati wa Passover ilikuwa ni jibu kwa mmoja wa wasikilizaji wake,mtu kutoka Damascus. Yule mtu alimuuliza Yesu;''Lakini,Rabbi,tutafahamu vipi kwa uhakika kwamba wewe umeletwa na Mungu,na kwamba kweli tunaweza kuingia katika huu ufalme ambao wewe na wafuasi wako mnasema uko karibu?''Na Yesu akajibu;

  '' Kuhusu ujumbe wangu na mafundisho ya mitume wangu,myahukumu kwa matunda yake. Kama sisi tunawaeleza kweli za roho,roho itashuhudia mioyoni mwenu kwamba ujumbe huo ni sahihi. Kuhusu ufalme na uhakika wako wa kukubalika na Baba wa mbinguni,nauliza baba gani kati yenu ambaye anastahili na ni mwema ambaye anaweza kumfanya mtoto wake awe na mashaka au wasiwasi kuhusu hali yake katika familia au nafasi yake ya usalama katika upendo wa moyo wa baba yake? Je,ninyi baba wa duniani mnaona raha kuwatesa watoto wenu na mashaka kuhusu nafasi yao ya upendo katika mioyo yenu ya kibinadamu? Hivyo,hivyo,Baba yenu wa mbinguni hawaweki katika mashaka watoto wake wa imani kuhusu nafasi yao katika ufalme. Mkimpokea Mungu kama Baba yenu,basi kwa hakika na kwa kweli ninyi ni watoto wa Mungu. Na kama ninyi ni watoto,basi mtakuwa na hakika katika nafasi yenu kuhusu yote yanayohusu kuwa milele watoto watakatifu. Ukiamini maneno yangu,kwa kufanya hivyo,unamwamini Yule aliyenileta,na kwa kumwamini Baba namna hiyo,unaifanya nafasi yako kama raia wa mbinguni kuwa ya uhakika. Ukiufanya utashi wa Baba mbinguni,hautashindwa kuupata uzima wa milele wa maendeleo katika maisha ya ufalme wa kitakatifu.

  ''Roho wa Kazi[Supreme Spirit,Roho wa Uzoefu,experience, anayefikiwa siyo kwa kuwa mwema ila kwa kutenda mema]atakuwa shahidi wa roho zenu kwamba ninyi kweli ni watoto wa Mungu. Na kama ninyi ni watoto wa Mungu,basi mmezaliwa na roho ya Mungu;yoyote aliyezaliwa katika roho anayo ndani yake uwezo wa kushinda mashaka yote,na huo ndio ushindi ambao unaondoa wasiwasi wote,yaani imani yako.

  ''Alisema Nabii Isaya,alipokuwa anazungumzia hizi nyakati;''Roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu,ndipo kazi ya haki itakapokuwa amani,utulivu na uhakika milele. Na kwa wale wanaoiamini hii injili kwa dhati,nitakuwa dhamana yao kwamba watapokelewa katika huruma za milele na uzima wa milele wa ufalme wa Baba yangu. Ninyi,kwa hiyo,mnaosilikiliza hizi habari na kuiamini hii injili ya ufalme ni watoto wa Mungu,na mnao uzima wa milele na ushahidi kwa dunia yote mmezaliwa katika roho ni kwamba mnapendana kwa dhati.''

  Makundi ya wasiklilizaji yalibakia saa nyingi na Yesu,wakimuuliza maswali mengi na kuyasikiliza kwa makini majibu yake. Hata mitume walipata ushupavu zaidi kuihubiri injili,kwa uweza mkubwa na kwa uhakika. Huu uzoefu walipokuwa Jerusalem uliwasaidia wale kumi na mbili. Ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kukutana na makundi makubwa kama haya,na walijifunza masomo mengi ya thamani ambayo yaliwasaidia sana katika kazi yao ya baadaye.
   
Loading...