Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Wakuu salamu.
Tumeshuhudia juhudi kubwa iliyofanywa na dola kupandikiza mgogoro ndani ya CUF, mgogoro uliolenga kumpoteza na kummaliza kisiasa Maalim Seif Shariff Hamad. Kilele cha mgogoro huo ni matukio yaliyofuatana kwa karibu (si kwa bahati mbaya) mkutano mkuu wa CUF Lipumba, na maamuzi ya Mahakama Kuu ya kumtambua Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF. Haya yote mawili yameshangiliwa sana na wanalumumba.
Yaliyofuata baada ya hapo, Lumumba imepigwa na butwaa, baada ya Maalim Seif na wanaomuunga mkono KUTUPA MZIGO, na kuhamia ACT Wazalendo. Tukio hili laweza kufungua ukurasa mpya kwa upinzani Tanzania, jambo ambalo Lumumba ni habari mbaya.
Kwenu ACT Wazalendo, na kwenu CHADEMA, mtambue kuwa vita mpya ya CCM SASA, si tena ndani ya CUF (mbaya wao hayupo tena). Hofu ya Lumumba ni uhusiano wa kisiasa Kati ya CHADEMA na ACT.
Tutarajie nyuzi nyingi humu za kuwafitinisha viongozi wa vyama hivi viwili, ikiwa ni pamoja na kufufua tofauti zao za zamani. Tutarajie siasa za majitaka dhidi ya Mbowe, Maalim na Zitto. Tutarajie uchonganishi wa CCM Kati ya Zitto na Maalim. Tutarajie propaganda za udini zirudi. CCM hawawi na raha iwapo upinzani hakuna mgogoro.
Kwa wapenda mabadiliko, propaganda hizo tusizishangae, na zisituyumbishe. Tushikamane zaidi na kusonga mbele.
Aluta Continua...
Sent using Jamii Forums mobile app