Kesi za viongozi wa CHADEMA

Kesi za viongozi wa CHADEMA

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
1,241
Reaction score
253
Kuna kesi kadhaa zilifunguliwa dhidi ya viongozi wa CHADEMA. Moja ya kesi hizo ni ile inayohusu kuandamana Arusha na nyinginezo.

Lakini ni muda sasa haijasikika kutajwa mahakamani. Je ni janja ya watawala kuzichelewesha kesi hizo kuzitolea hukumu kwa manufaa yao kisiasa?

Watawala wanaweza kutoa hukumu kwa viongozi wa CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu ujao ili kuwafanya wasiwe na sifa ya kugombea.
 
Serikali dhaifu ndiyo faida yake hiyo. Wanaochofanya ni mambo ya mwaka 47 na mbinu zao tunazitambua mapema sana!
 
Bado wana kesi nyingi wanavifanyia kazi! wana kesi za Epa, Kagoda, Meremeta, na zile za elephant bluethoth
 
bado wana kesi nyingi wanavifanyia kazi! Wana kesi za epa, kagoda, meremeta, na zile za elephant bluethoth

kesi zenyewe wanaogopana kwa kuwa wanajuana kuwa ni wao wenyewe wahusika wa ufisadi huo.
 
Kaka moja haikai wala mbili haikai. Kila maamuzi upande wa pili ni moto. Ndio maana wanasemaga UPEPO TU UNAPITA ikizidi LIWALO NA LIWE.
 
Ngoja wazipige danadana na ikifika 2015 waanze kuzipeleka mchaka mchaka ili wakipatikana na hatia uchaguzi wasahau.. ndio bomu hilo litakalo tenguliwa uchaguzi ukikalibia...maana hawana njia nyingien zaidi ya hizo za kutumia mahakama..
 
CDM inabidi kuwa makini sana na hili...magamba waweza kuja na hukumu za ajabu mapema mwaka 2015 ili kuathiri uchaguzi mkuu kwa upande wa cdm
 
Kaka moja haikai wala mbili haikai. Kila maamuzi upande wa pili ni moto. Ndio maana wanasemaga UPEPO TU UNAPITA ikizidi LIWALO NA LIWE.

Ndg yangu malaka umenena ukweli, ni vile tu wachunguzi wetu wa jf hawajapata data za ndani kuhusiana na kesi hizo. Laiti tungejua jinsi wanavyo-gongana vichwa huko, kila mmoja akijaribu kijinusuru na shari kamili..!!!
Nahisi panapotokea tafrani ktk kutokukubaliana, mameno ya "UKIMWAGA UGALI, MIMI NITAMWAGA MBOGA" huwa kitulizo chao kabla ya :UPEPO TU UNAPITA ikizidi LIWALO NA LIWE". Ila naamini, siku si nyingi, huo ugali wao na mboga itamwagwa na wasiyemdhani na kwa namna wasiyoitarajia.
 
Kaka we ngoja mfano wa hiyo ya "kumwaga mboga ukimwaga ugali" ni pale White Hair au watu wake wasipoingia CC. Picha tamu balaa wangu wewe stay tune tu utaona.
 
This is a valid argument, it must be noted for those in question.
 
Kama wanaacha wawaathiri makamanda 2015 ktk hukumu zao kwa hakika Uchaguzi hautafanyika
 
Kwa taarifa ambazo nilizipata ni kuwa wakili msomi Method Kimomogoro alifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, akitumia Sheria ya Basic Rights n Duties Act ya mwaka 1994 kusimamisha kesi zote ambazo zina sura ya ubambikaji wa kisiasa. Imeshasikilizwa mara moja na bado itaendelea...............
 
That's a good move.
 
Kuna kesi kadhaa zilifunguliwa dhidi ya viongozi wa CHADEMA. Moja ya kesi hizo ni ile inayohusu kuandamana Arusha na nyinginezo.

Lakini ni muda sasa haijasikika kutajwa mahakamani. Je ni janja ya watawala kuzichelewesha kesi hizo kuzitolea hukumu kwa manufaa yao kisiasa?

Watawala wanaweza kutoa hukumu kwa viongozi wa CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu ujao ili kuwafanya wasiwe na sifa ya kugombea.

Hata kama Watawahukumu wakati wa Uchaguzi, haitasaidia kitu! Wakumbuke kuwa Upepo wa mabadiliko ni mkali sana. Wakifanya hila hii basi wajue kuwa hasira ya wananchi itapanda mara dufu, watapoteza kabisa mvuto na upinzani utashinda tu 2015! Hazina ya Ushindi wa Chadema iko kwenye fikra za wananchi ambao ndio wapiga kura. Nguvu ya Chama cha Magamba iko kwenye Ufisadi, utapeli, Unyang'anyi wa Mali ya Umma na Matumizi mabaya ya polisi, Mahakama na Bunge! Chama cha Matapeli kinanuka na hila zao tumeshazijua!
 
hata kama watawahukumu wakati wa uchaguzi, haitasaidia kitu! Wakumbuke kuwa upepo wa mabadiliko ni mkali sana. Wakifanya hila hii basi wajue kuwa hasira ya wananchi itapanda mara dufu, watapoteza kabisa mvuto na upinzani utashinda tu 2015! Hazina ya ushindi wa chadema iko kwenye fikra za wananchi ambao ndio wapiga kura. Nguvu ya chama cha magamba iko kwenye ufisadi, utapeli, unyang'anyi wa mali ya umma na matumizi mabaya ya polisi, mahakama na bunge! Chama cha matapeli kinanuka na hila zao tumeshazijua!

lazima wapenda haki demokrasia na maendeleo tujipe moyo. Ushindi ni lazima.
 
naomba chadema muwafatilie kwa karibu washtakiwa wa kesi zenu mfano huku mafinga washtakiwa hawna sapoti ya chama jitahidi sana wananchi bado wanawaamini

hebu wapigie simu makao makuu. Namba zao zipo
 
Back
Top Bottom