Kesi za Mafisadi zitakuwa za Mwendokasi. Hazitazidi miezi 9

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,780
JAJI Mkuu, Mohammed Chande Othman, amesema Mahakama Maalumu ya Uhujumu Uchumi na Ufisadi itaamua kesi kwa muda usiozidi miezi tisa na kwamba itaanza na majaji 14.

Aidha, wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14 watakaofanya kazi katika mahakama hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye Chuo cha Mahakama Lushoto mkoani Tanga, ili kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa mahakama hiyo.

Jaji Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu huo.

Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora kuliko miaka mingine.

Alisema baada ya sheria hiyo ya uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Jaji Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais kutoa idhini ya sheria hiyo na baadaye kupitishwa kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze kutumika.

Alieleza kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti hilo la Serikali, Jaji anatakiwa kutunga kanuni mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi kutokana na kuwa sheria hiyo inahusu makosa makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa na uhujumu uchumi.

“Tuko mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha mashahidi wanalindwa. Jengo la mahakama hii litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na Mlimani City na tayari tumepeleka wasajili watendaji,” alisema.

Mwishoni mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa majengo ya mahakama hiyo yatakabidhiwa leo. Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa majengo hayo.
Alisema wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo juu ya namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.

Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Source: Mpekuzi
 
Hivi fisadi ni yupi??Mbona huu mtego wanajiundia ukilipuka unaanzia magogoni hadi shida.
 
Ukiweka time limit kwa vitu kama hivi, ambavyo ni a bit too technical, kuna hatari ya kutoa maamuzi ya kulipua and this brings fear that justice might be compromised due to rush. Let us wait and see rather than speculate!
 
Tatizo sio kuwa na mahakama hiyo Bali weledi wa waendesha mashtaka. Kama wataendelea kufanya kazi zao kwa kukurupuka hiyo mahakama itakuwa ni upotevu wa pesa tuu.
Tukumbuke mahakama inasimamia haki hivyo kama ushahidi unaletwa wa hovyo kila kesi itapigwa chini
 
Mlibeza sana kuwa Mahakama hiyo haiwezi kuanzishwa. Imeanzishwa mmeanza kubadili gia angani
 
Mambo mengi namuunga mkono mzee wa majipu kasoro vitendo vyake vya kukandamiza demokrasia
 
Usizunguushe Watanzania akili.Maana ya fisadi iko wazi.Kama wewe hujui tafuta kamusi ya kiswahili.Sisi walala hoi tunajua maana ya fisadi kwa kuwa wametuumiza sana.Huwezi kujua maana ya fisadi kama wewe ndiye uliyefisidi.
Hivi fisadi ni yupi??Mbona huu mtego wanajiundia ukilipuka unaanzia magogoni hadi shida.
 
Tatizo sio kuwa na mahakama hiyo Bali weledi wa waendesha mashtaka. Kama wataendelea kufanya kazi zao kwa kukurupuka hiyo mahakama itakuwa ni upotevu wa pesa tuu.
Tukumbuke mahakama inasimamia haki hivyo kama ushahidi unaletwa wa hovyo kila kesi itapigwa chini
Malengo yake ni mazuri lakini??? NACHELEA TU, ISIJE SEMINA IKAWA ELEKEZI KUWA LAZIMA WAFUNGWE! WAPATIKANE NA HATIA TU WHATEVER THE EVIDENCE! One is driven to think in that direction from the insistence on the establishment of the same! Hopefully this will not happen.
Secondly the competence of Judges. Nakumbuka issue ya Lisu na majaji! see attachment!
Usizunguushe Watanzania akili.Maana ya fisadi iko wazi.Kama wewe hujui tafuta kamusi ya kiswahili.Sisi walala hoi tunajua maana ya fisadi kwa kuwa wametuumiza sana.Huwezi kujua maana ya fisadi kama wewe ndiye uliyefisidi.
Hapo pa red please-Ikiwepo hiyo mahakama kama mtoto wako yuko shule ya kata watatoka huko au kuwa shule nzuri, huna kazi utapata kazi? Madawa hospitalini hakuna yatapatikana etc! Sidhani kama mafisadi ndio waliokuumiza, ni mfumo uliopo, na bado hao hao wenye mfumo wako serikalini! Tafakari
 
Attachments

  • Majaji VIHIYO.doc
    79 KB · Views: 313
Wafia chama ni watu wa ajabu sana "Naangalia wale wanavyoliwa mwisho na pata jibu kuwa uelewa wao ni mdogo na hapo mpaka wanaliwa nikuwa wamewaza mpaka wakafikia mwisho wakufikiri,sasa panakuwa hakuna options nyingine!" Hivyo wafia chama wamefikia mwisho kuwaza....Hivi kwa hiyo akili ndogo mliyopewa kwenye kisoda mnaamini kuwa fisadi ni Lowassa basi??Mungu awarehemu wafia chama nchi imemalizwa na mfumo wa chukua changu mapema leo Tanzania mnaona fisadi ni Lowassa,hamuoni akina Mkono hadi ofisi zimefungwa,chenge etc....kweli Nyumbu kazaliwa kuliwa na simba na chui basi!!
 
Hehehe...kama itahusika pia na kesi za ugaidi basi sasa ni wazi Jaji Dkt Feleshi ni miungoni mwa jopo hilo maana ni miungoni mwa wale wataalamu watatu walopelekwa kozi na kuanziasha mchakato wa sheria ya ugaidi, I am super excited maana watajuta vile hahongeki yule jamaa.
 
Natarajia kufungua kesi dhidi ya raisi wa awamu ya tatu nne na tano kesi kubwa za ufisadi
Tegeni masikio yenu nn kitatokea
 
JAJI Mkuu, Mohammed Chande Othman, amesema Mahakama Maalumu ya Uhujumu Uchumi na Ufisadi itaamua kesi kwa muda usiozidi miezi tisa na kwamba itaanza na majaji 14.

Aidha, wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14 watakaofanya kazi katika mahakama hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye Chuo cha Mahakama Lushoto mkoani Tanga, ili kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa mahakama hiyo.

Jaji Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu huo.

Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora kuliko miaka mingine.

Alisema baada ya sheria hiyo ya uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Jaji Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais kutoa idhini ya sheria hiyo na baadaye kupitishwa kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze kutumika.

Alieleza kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti hilo la Serikali, Jaji anatakiwa kutunga kanuni mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi kutokana na kuwa sheria hiyo inahusu makosa makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa na uhujumu uchumi.

“Tuko mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha mashahidi wanalindwa. Jengo la mahakama hii litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na Mlimani City na tayari tumepeleka wasajili watendaji,” alisema.

Mwishoni mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa majengo ya mahakama hiyo yatakabidhiwa leo. Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa majengo hayo.
Alisema wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo juu ya namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.

Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Source: Mpekuzi
hawa watu wanashangaza kweli. badala mahakama iwe karibu na ukonga au segerea au keko au hata karibu na isanga dodoma wao wanaipeleka pale mlimani city. ajabu hii.
 
Ukiweka time limit kwa vitu kama hivi, ambavyo ni a bit too technical, kuna hatari ya kutoa maamuzi ya kulipua and this brings fear that justice might be compromised due to rush. Let us wait and see rather than speculate!
mambo yako huwa atuyaamini.

swissme
 
Back
Top Bottom