Kesi za mabomu masasi utata mtupu

Kesi za mabomu masasi utata mtupu

MIRICHE

Member
Joined
Sep 18, 2012
Posts
20
Reaction score
8
ndugu wana JF,


Naomba kwa mara ya kwanza niwahabarishe kile kinachoendelea kwenye Mahakama ya Wilaya Masasi,hususani kesi zinazohusiana na vurugu zilizotokea tareehe 26/01/2013,maarufu kama kesi za MABOMU.kwa kifupi vurugu hizo zilianzia kwenye kituo kikuu cha polisi hapa masasi,kati ya madereva pikipiki maarufu kama BODABODA na Mkuu wa polisi wa wilaya masasi,kamanda wa polisi wa barabarani na mkuu wa upelelezi wa wilaya,baada ya maafisa hao watatu kukataa kuwasikiliza waendesha pikipiki hao juu ya kero yao kubwa kuhusu TRAFIKI NA POLISI WA DORIA maarufu kama TIGO.
Mwihso wa siku zilitokea vurugu kubwa kituoni hapo na zikasambaa mji mzima na kusababisha uharibufu mkubwa wa mali za uma na watu binafsi.maafisa hawa baada ya kugundua kuwa wamefanya kosa kubwa wakageuza kibao na mara moja wakahusisha vuragu hizo na GESI,hivyo chama kinachoonekana kukua kwa kasi hapa masasi (CHADEMA) kikahusishwa na na vurugu hizo na hivyo baadhi ya viongozi wa chama hicho kukamatwa na kufunguliwa kesi za UCHOCHEZI.(mbuni kuficha kichwa chini)

kosa lingine walilofanya polisi ni kukamata wapita njia na watu ambao walifika maeneo ya matukio kushangaa kilichotokea na kuwaacha wahusika wakuu ambao ni madereva pikipiki.Hili wamefanya makusudi kwani hapa masasi pikipiki nyingi zinamilikiwa na Askari polisi kama chanzo chao kujipatia kipato.kwa mfano Askari mmoja kwa jina la KOMBA(AMEHAMISHWA)Alikuwa ana miliki pikipiki saba.

Tukirejea mahakamani tangu mwezi wa kwanza hadi leo ni danadana tu,na sasa wamebuni mtindo mwingine,KESI zinafutwa halafu watuhumiwa wanakamatwa tena.Na taarifa kutoka ndani ya mahakama zinasema kuwa ni mpango wa kuta kukusanya pesa kutoka kwa watuhumiwa baada ya kugundua kuwa wengi waliowakamata hawana ushahidi nao.mfano tarehe5/09/2013 kesi namba 84 ilifutwa na watuhumiwa walikamatwa tena na baada ya kufunguliwa mashtaka upya mtuhumiwa mmoja kwa jina la ISSA MWEMBE aliachiwa baada ya kutoa kitu kidogo,na taarifa kutoka nndani ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara anaurafiki na mpelelezi wa wilaya ngugu JOSHUA MAFILANGO

kubwa zaidi watuhumiwa wameanza kupata hofu juu ya kutendewa haki mahakamani hapo kwani zinasema kuwa hakimu wa wilaya kwa jiana la mama NYEMBELE na ofisa upelelezi wa wilaya bwana JOSHUA MAFILANGO ni ndugu wa karibu ambao wanatoka mkoa mmoja(MBEYA) na kijiji kimoja,pia ndugu JOSHUA MAFILANGO ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya HARUSI ya mama nyembele ambaye ni hakimu wa wilaya ya masasi.
Taarifa zingine zinasema kuwa mahakimu wameanza kujitoa kwenye baadhi ya kesi kwa vigezo kuwa hawpo huru katika kutenda haki,na hata mahakimu wengine kutoka Tandahimba na Newala ambao wamepangiwa kesi hizo huu ni mwezi wa nne tangu wapangiwe kesi hizo hawajafika hivyo kufanya kesi kutajwa tu kila tarehe inapofika.

Hivyo ndugu wana JF tunaomba kulika sakata hili ili rai wasio na hatia waweze kutendewa haki.
 
Back
Top Bottom