Kesi za barabarani; Trafiki bongo wamepewa mamlaka makubwa mno wakiamua wanaweza hata kukutandika makofi na usiwafanye kitu kama huna ushahidi

Waelekezwe washughulike na Makosa ya wazi kama ubovu wa Gari, BIMA, usajili n.k, wajikite kufanya kazi zenye ushahidi siyo Makosa ya kuviziana!
Hivi kiuhalisia, Bima ya gari inastahili kufuatiliwa na hawa polisi wa trafic?
 
Hiyo ndio maana ya watanzania wanyonge,tukiukataa unyonge hayo mambo yataisha .
 
Shida iko kwenye sheria na utaratibu.

Kama kweli wanalinda mali na watu, palipaswa kuwa na utaratibu mahususi katika hili kama vile:-

Kwenye kila station pawe na Polisi, SUMATRA/LATRA, mwakilishi wa madereva, mwakilishi wa wamiliki wa magari na mwakilishi wa raia.

Ujinga wote wa hao jamaa usingekuwepo wala malalamiko juu yao
 
unawajua SUMATRA au unawasikia.

kawaulize madereva wa daladala,kama hawajakutukana.

wao wakikushika,unaenda yard zao,kutoa gari getini ni mpaka ifaulu mitihani yote,ukipona sana milioni 5 imeenda.
 
Polisi wengi ni wazembe na wana maadui wengi. Ni rahisi kumuumiza na kuwaachia ujumbe waache ufala....

Kuna mwenzao alipigwa risasi sayansi kisa unoko
unaua traffic kisa kachukua elfu 10 yako.wewe ua uone kama kushikwa itahitaji FBI kama kwa wengine,ndipo hapo utajua damu ni damu maji ni maji.

gari lako,hela yako,akili yako,muda wako.lakini barabara ina wengi mkuu.
 
Wamepewa malengo ya makusanyo as if serikali inainjoi ongezeko la makosa ya barabarani.
 
unawajua SUMATRA au unawasikia.

kawaulize madereva wa daladala,kama hawajakutukana.

wao wakikushika,unaenda yard zao,kutoa gari getini ni mpaka ifaulu mitihani yote,ukipona sana milioni 5 imeenda.
Siku zote mhalifu huogopa kupita karibu na Polisi, ila kama wote wapo pale usawa utazingatiwa maana kila mwakilishi atatoa maoni yake kabla ya hukumu kumpata dereva au mmiliki wa gari
 
Siku zote mhalifu huogopa kupita karibu na Polisi, ila kama wote wapo pale usawa utazingatiwa maana kila mwakilishi atatoa maoni yake kabla ya hukumu kumpata dereva au mmiliki wa gari
hamna maoni mzee,show ya SUMATRA ni baab kubwa.

ni sawa na wengine waliokuwa wakikamatwa na mawakala wa wrong parking,wakacheka wakidhani ni zile 30 za traffic,wakipewa recept ya 300k gari moja,wanadata.
 
Back
Top Bottom