Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 72
- 261
Naam, ndio kama mlivyosikia kupitia Vyombo mbalimbali vya habari, aliyekuwa mkuu wa wilaya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wameshinda rufaa Yao waliokuwa wakipinga hukumu ya miaka thelathini Jela baada ya kupatikana na hatia ya Unyang'anyi wa kutumia silaha.
Imeisha hiyo... Kama hutaki kanunue soda Peps baridi kunywa! [emoji23] [emoji23]
Sasa hiyo kwangu sio habari, of course nililitarajia hilo kwa sababu ambazo nilikwishawahi Kuzi andika hapa.
Shida yangu mimi ni moja tu, na ninaomba viongozi wangu wasikivu hili walichukue, japo najua kwa sasa vichwa vyao vinawauma na hawapati usingizi kwa sababu ya ishu ya Mafuta ba uchumi kwa ujumla.
Ipo hivi, huyu bwana Lengai Sabaya alikuwa mtuhumiwa kwa a watuhumiwa wengine tu. Katiba yetu inataka kwamba sisi wote ni sawa mbele ya Sheria.
Alishtakiwa kwa mara ya kwanza ilikuwa tarehe 28 June 2021, kesi yake ilisikilizwa harakaharaka na hatimaye tarehe 15/10/2021 alisomewa hukumu yake iliyomtia hatiani na kisha kupewa adhabu ya kwenda Jela miaka thelathini(30).
Yaani ni wastani wa miezi minne(4) tu kidume akawa ameshamaliza kesi yake. Hakuridhika, kidume kupitia wakili wake wakaweka nia ya kukata rufaa, hii ilikuwa tarehe 21/10/2021.
Leo hii tarehe 6/5/2022 hukumu ya rufaa yake imesomwa, kafurahia ushindi na ndugu zake mahakamani.
Ni jumla ya miezi Sita(6) tu jamaa kaimaliza rufaa yake na kutangaza ushindi na kufanya kesi yake yote kudumu jumla ya miezi kumi(10) na wiki kadhaa. Hongera kwake.
Sasa point yangu ni kwamba magerezani mpaka hivi unaposoma ujumbe huu Kuna wafungwa na mahabusu mamia ambao kesi hazisikilizwi au rufaa zao tangu walivyo weka nia ya kukata rufaa hata mwenendo tu wa kesi zao hawajapewa zaidi ya miaka miwili au zaidi.
Kuna wafungwa wengi ambao rufaa zao hazijapangiwa tarehe wala majaji wa kusikiliza licha ya kukamilika kwa nyaraka zote muhimu.
Wengi wakifuatilia hupewa majibu rahisi rahisi tu, mara fedha za kuendesha vikao vya majaji hazijatoka, au mwenendo ya kesi zao bado haijachapwa au ipo kwenye foleni ya kuchapwa zaidi ya mwaka au miaka.
Hii dhana ya Usawa mbele ya Sheria katika katiba tafsiri yake ninini kama kuna baadhi wanapewa kipaumbele kuliko wengine mbele ya Sheria.
Wale watoto wa masikini kule magerezani ambao majina Yao si makubwa nani awapiganie kuhakikisha kesi zao zinasomwa kuhukumiwa kwa wakati.??
Sisi wanasheria husema haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokataliwa, 'justice delayed is justice denied', ningekuwa na Sauti kubwa ningeamuru au kutoa tamko leo kuitaka idara ya mahakama ijitathmini kwa hii dhambi iliyopewa Jina la kesi zenye 'Public interest'.
Bado nipo na lundo la vitabu ninatafuta kifungu kinachoelekeza kesi za wanasiasa kukimbizwa na kupewa kipaumbele na mahakama. [emoji1787][emoji1787]
M. Majaliwa, esq.