barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Ile kesi ya malalamiko dhidi ya uchaguzi wa Jimbo la Iringa,iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM ndugu David Mwakalebela imetupiliwa mbali na Mahakama.
David Mwakalebela ameamuliwa kulipa ghalama za kesi na hivyo kuanzia leo Mh.Peter Msigwa ni mbunge halali wa Jimbo la Iringa Mjini.
David Mwakalebela aligombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini na akabwagwa chini na Mama Mbega ktk kura za maoni mara baada ya kukutwa akitoa "rushwa" kwa wanachama wa chama chake ktk kata ya Nduli,mwaka 2015 Mwakalebela alijitosa tena kugombea Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM akichuana vikali na makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa JescaMtavatavangu.
Wakili wa Mbunge Msigwa,Jane Masey anasema Mahakama imetupilia mbali kesi hiyo baada ya mlalamikaji kukosa hoja za msingi.