Kesi ya mtoto wa nyani kutolewa uamuzi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imepanga, Mei 31 mwaka huu kutoa uamuzi dhidi ya mshtakiwa Baraka Joshua(23) kama ana kesi ya kujibu au la.

Hatua hiyo imefikia baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Joshua maarufu kama mtoto wa nyani, aliishi na nyani baada ya kuzaliwa na kutupwa porini takribani miaka nane iliyopita katika pori lililopo mkoani Shinyanga, anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 9, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kimanga.

Hakimu Catherine Kiyoja anayesikiliza kesi hiyo alipanga Mei 31, mwaka huu kutoa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au laa.


Chanzo: Mwanachi
 
Tuwekee na picha kidogo ya huyo mtoto wa Monkey. Wengine huku mikoani hatumfahamu au huko Dar ni Celebrity kama Harmorapa!?
 
Back
Top Bottom