Mahakama yatupilia mbali Afande Fatma kusomewa mashtaka popote alipo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Kesi inayomkabili 'Afande' Fatma Kigondo, anayeshtakiwa kwa kuratibu ubakaji na ulawiti wa kundi dhidi ya binti wa Yombo, Dovya jijini Dar es Salaam, imeendelea Oktoba 18, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Nyamburi Tungaraja, ametupilia mbali maombi ya upande wa mlalamikaji yaliyotaka mshtakiwa asomewe mashtaka popote alipo, akisema maombi hayo hayajakidhi vigezo vya kisheria.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya Jumatano, Oktoba 16, 2024, upande wa mlalamikaji kuwasilisha ombi hilo, ambapo Hakimu Tungaraja aliahidi kupitia sheria kabla ya kutoa maamuzi ya kusaini au kutosaini hati ya mashtaka kama ilivyoombwa.

Inafahamika kuwa Fatma Kigondo amekuwa akishindwa kufika mahakamani kwa madai ya kuugua. Hii hapa video ya Mwanasheria upande wa mlalamikaji akimwakilisha Wakili Peter Madeleka, akielezea maamuzi hayo.

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom