Kesi ya Mdude kuamuliwa Julai 9, 2025

Kesi ya Mdude kuamuliwa Julai 9, 2025

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
Gusf1oNXgAAu0Y8.jpg

Kesi ya Habeaus Corpus iliyofunguliwa na Sije Emmanuel Mbugi, mke wa kada wa Chadema, Mpaluka Mdude Nyagali ilishikilizwa Juni 30 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Mbeya.

Mdude alitekwa nyumbani kwake Mei 2 usiku na watu wasiojulikana, ambapo kabla ya kumchukua walimpiga na kumjeruhi.

Soma zaidi: Chadema, kambi ya kumtafuta Mdude

Jeshi la Polisi lilikanusha kumchukua Mdude na likasema linafanya uchunguzi lakini mpaka sasa hakuna taarifa iliyotolewa.

Akifafanua undani wa shauri hilo, Wakili Boniface Mwabukusi, anayewaongoza mawakili wenzake Hekima Mwasipu na Solomon Kimunyu amesema, “Habeaus Corpus maana yake ni ulete mwili mbele ya mahakama. Kwa hiyo tunawataka tunaowashitaki kuuleta mwili mbele ya Mahakama.

Mwabukusi ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), amesema uamuzi wa shauri hilo utatolewa Julai 9, 2025.
 
Hii ndio taasisi tunazozitaka. Sio taasisi inasikilizia kwanza Rais anatakaje
 
Sema tu watanzania wamezidi uoga ndiyo maana polisi wanatenda uhalifu waziwazi na kujifanya hawajatenda huo uhalifu.Inatakiwa tuwe kama wakenya.polisi wa Kenya walimteka na kumuua mkenya na kusababisha Nchi kunukishwa na wakenya Hadi polisi kukili kuua na kufungwa.Watanzania acheni uoga.Haki ikishindikana kupatikana Kwa njia ya amani hutafutwa Kwa njia ya vutugu.Aluta continua
 
Kwa hawa mburula wa tanganyika siyo uoga tu ili ubinafsi wa kishamba!! Waachwe wafe na wajitetee wenyewe tu stupid
 
Back
Top Bottom