Kesi ya Lissu yakwama kuendelea Kisutu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imeshindwa kuendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu wakili wa Serikali anayeindesha, Mohammed Salum amepangiwa kazi nyingine.

Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa ameiambia mahakama leo Ijumaa kuwa kesi ilipangwa kusikilizwa lakini wakili Salum anayeiendesha amepangiwa kazi nyingine hivyo akaomba iahirishwe.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, kesi imeahirishwa hadi Juni 16, 2017.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chadema anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Anadaiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa:

“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Katika kesi hiyo, tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Kimweli na Staff Sajenti Ndege wamekwishatoa ushahidi wao.
LISSU+PICHA.jpg
 
Huyo wanampangia kazi nyingine ili asiendelee kupewa za uso na kuishia kusema hapana
 
Duu hizi kesi hizi!! Jana nimepata habari kwamba kesi zote ambazo Lisu anaishinda Serikali tumekua tunamlipa fidia ya mamilion ya pesa. Sasa nimegundua naye Lisu kapata njia ya kula pesa ya Serikali kwa style yake, yaani amekua anatoa matamshi kijanja sana huku akijua kabisa kwamba kuna wakurupukaji watamburuza mahakamani ambako anawashinda vibaya alafu analipwa fidia then anakula na familia yake, kweli nchi hii usipokua mjanja wa kuchungulia fursa utaendelea kuwa masikini. Sijui na mimi niseme Magu mjinga ili wanikamate then nikawashinde mahakamani? any way ngoja niache nisije nikapotea
 
MWANA SHERIA MKUU CHADEMA.

Na ZUMA anamtambua vizuri tu

Swissme
 
Duu hizi kesi hizi!! Jana nimepata habari kwamba kesi zote ambazo Lisu anaishinda Serikali tumekua tunamlipa fidia ya mamilion ya pesa. Sasa nimegundua naye Lisu kapata njia ya kula pesa ya Serikali kwa style yake, yaani amekua anatoa matamshi kijanja sana huku akijua kabisa kwamba kuna wakurupukaji watamburuza mahakamani ambako anawashinda vibaya alafu analipwa fidia then anakula na familia yake, kweli nchi hii usipokua mjanja wa kuchungulia fursa utaendelea kuwa masikini. Sijui na mimi niseme Magu mjinga ili wanikamate then nikawashinde mahakamani? any way ngoja niache nisije nikapotea
Onesha ushahidi ya unachokisema
 
Back
Top Bottom