Kesi ya Lissu (udikteta uchwara) yapigwa kalenda hadi April 03

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,886
=

















Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Kwa ufupi
  • Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa imeahirishwa kwa sababu yupo likizo.
  • Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Dar es Salaam. Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.

Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa imeahirishwa kwa sababu yupo likizo.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, Lissu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa:“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’
 
Shahidi alishasema hamjui dikteta uchwara na pia hajui maana ya dikteta uchwara na alienda mbali zaidi kwa kusema ni halali kuipinga serikali iliyopo madarakani katika nchi ya demokrasia ya vyama vingi, alipoulizwa iwapo neno dikteta ni la kisiasa akakubali, hii maana yake jamhuri wameshindwa thibitisha makosa naona mwisho ni DPP kuiondoa hii kesi mahakamani
 
Shahidi alishasema hamjui dikteta uchwara na pia hajui maana ya dikteta uchwara na alienda mbali zaidi kwa kusema ni halali kuipinga serikali iliyopo madarakani katika nchi ya demokrasia ya vyama vingi, alipoulizwa iwapo neno dikteta ni la kisiasa akakubali, hii maana yake jamhuri wameshindwa thibitisha makosa naona mwisho ni DPP kuiondoa hii kesi mahakamani
DPP hana watu kabisa
 
Come to think of it.... may be kosa ni neno uchwara.... kinyume chake (si kwa Kiswahili fasaha tho) ni halisi.... labda Mh. Lissu angetumia neno Dikteta Halisi asingekuwa na kesi. hahah Tanzania ya viwonder
 
Back
Top Bottom