GE2025 Kesi ya Lissu kuendelea leo Oktoba 24, shahidi wa nne wa jamhuri asubiriwa kwa hamu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Shahidi wa Tatu (3) wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Samwel Elibariki Kaaya amemaliza kutoa ushahidi wake hapo jana

Leo, Ijumaa Oktoba 24.2025, kesi hiyo inayosikilizwa mfululizo kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru inaendelea tena

Pamoja na mambo mengine, inawezekana upande wa Jamhuri ukamleta Mahakamani leo shahidi wa Nne (4) ili aanze kutoa ushahidi wake, lakini pia huenda Jamhuri ikaja na taarifa nyingine, hiyo ni kutokana na maelezo waliyotoa Mawakili wa Jamhuri Mahakamani hapo jana wakati wakiomba hairisho ambapo ilinukuliwa wakieleza kuwa licha ya kwamba shahidi wa tatu (3) amemaliza kutoa ushahidi wake, lakini pia wanaenda kutafakari kuhusiana na 'maamuzi madogo' yaliyotolewa na Mahakama katika mwenendo wa kesi hiyo

Maamuzi hayo ni yale yanayohusu mapingamizi mawili tofauti yaliyokuwa yamewekwa na mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, mapingamizi ambayo yote yakikubaliwa na Mahakama kwa nyakati tofauti.
 
Mambo yasiwe mengi, kesi ya mwisho watangaze itakuwa ni baada ya rais kuapishwa ili jamaa akapumzike zake kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…