PostGE2025 Kesi ya kupinga tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29 inaendelea leo Desemba 10

PostGE2025 Kesi ya kupinga tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29 inaendelea leo Desemba 10

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Leo, Jumatano Desemba 10.2025 kesi Na. 30210/2025 iliyofunguliwa na Mwanaharakati Rosemary Mwakitwange na wenzake wawili (2) ambao ni Mawakili Deogratias Mahinyila na Edward Heche dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wajumbe Nane wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29 mwaka huu na siku zilizofuata na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) inakuja kwa ajili ya kutajwa mbele ya Jaji Hussein Salum Mtembwa.

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

1765347935687.png
Kesi hiyo inahusu kupinga uteuzi wa Tume ya Uchunguzi inayoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Othman Chande Othman, ambapo miongoni mwa kubwa za kupinga tume hiyo ni madai ya kutokuwa huru, kuundwa kinyume na sheria, madai ya kuundwa tume hiyo kwa nia mbaya, tume kukosa mantiki ya kisheria kwa uundwaji wake nk,

Waombaji wameomba Mahakama itengue uteuzi huo kwa kukosa sifa na pia mamlaka za uteuzi zisiunde tume yenye muundo huo unalalamikiwa na aleta maombi.
 
Back
Top Bottom