Kesi Ya khanga(Monica)

Francis Mawere

JF-Expert Member
Nov 17, 2015
958
830
Mtunzi : Fredy Ndalakasheba
Msimulizi:Maestro KingKikii

Mama nipe Nauli nikamfuate monica Eeh,
Amekimba Zambia na Treni ya Mizogo Eeh,
Kisa cha kukimbia madeni yamemzidi Doti 10 Za Khanga alizokopa hajalipa,
Anatafutwa na Polisi popote apatikane, Na mimi rafiki yake nko nje kwa Dhamana,
Nililala Rumande siku mbili kituoni, usumbufu nilioupata kwa kweli sina Raha,

Naona Bora niende Zambia Nkamtafute Monica,
Nimulete Daresalam apambane na kesi yake,
Wee Monika aieeee uko wapi Eeeh?

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi
Asipofika nitapelekwa jela kutumikia Kifungo,

Naona Bora niende Zambia Nkamtafute Monica,
Nimulete Daresalam apambane na kesi yake,
Wee Monika aieeee uko wapi Eeeh?
 
Umenikumbusha mbali sana. Dingi alienda dar kikazi aliporudi mkoa kaja na radio casseti aina ya nova..akiwa na hiyo casseti ya ndala kasheba akiwa amevaa pama kubwaa... Pia alikuja na casseti ya vunja mifupa duh ilikua raha sana... Nikilewa pombe navunja vikombe
 
:D:D Enzi hizo Ladha ya Muziki ilikua ikifahamika Vilivyo. Wako wapi Rainbow wazee wa MILIMA YA KWETU, Yuko wap Maestro King Kikii, wako wako wapi Kilwa Jazz, ni nani atakae rudisha Homa za Mkali Fredy Ndalakasheba, Ni nani anirudishie Marijani Rajab, nk????????
 
Ni nani ataigusa Mikono ya Emma Mkello na Eddy Sheggy.. juu ya Rhythm Guitar??????
 
Back
Top Bottom