Kesi ya Kafulila yaahirishwa tena

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,188
570
Akiwa tayari ameitwa na Jaji, Mlalamikaji kwenye kesi ya uchaguzi David Kafulila dhidi ya Hasna Mwilima Mbele ya Jaji Ferdinand Wambari alikabiliwa na pingamizi lililopelekea kesi kuahirishwa Leo mchana mpaka alhamis machi31. 2016.

Pingamizi hilo liliwekwa na wakili wa Mhe Hasna Mwilima, Msomi Kennedy Fungamtama kwamba hati ya kiapo ya Mhe Kafulila ina kasoro kwa hoja kuwa haikuzingatia utaratibu wa kiapo ambapo ilikosa maneno "naapa kwamba ushahidi ninaotoa ni ukweli, kweli tupu, Mungu nisaidie".

kosa jingine kwamba hati ya kiapo ya Mhe Kafulila haikutolewa nakala kwa mawakili wengine na badala yake zikawekwa nakala halisi.

Katika utetezi wake, mawakili wa Kafulila, Prof Safari, Daniel Lumenyera na Msomi Kagashe. waliambia mahakama kwamba kwanza, kuhusu kuleta nakala halisi badala ya kopi haina madhara kwa mahakama na wala upande wowote zaidi ni kwamba ushahidi wa nakala halisi una nguvu zaidi kuliko kopi.
Na kuhusu utaratibu wa kiapo, mawakili hao wa Mhe KAFULILA walisisitiza kuwa hoja kama hiyo ilitolewa na mawakili haohao kwenye hatua za awali za kesi hii Disemba 2015, ambapo Mhakama Kuu iliamua kuwa kiapo kwa kutumia hati hakiwezi kuandikwa kama kiapo cha shahidi anapozungumza mahakamani. mawakili hao wa Kafulila walikwenda mbali zaidi na kusema uamuzi wa mawakili hao kurudisha hoja ilokwishakuamuliwa na mahakama hiyo hiyo nisawa na kuitega mahakama kuona kama inaweza kutoa maamuzi tofauti kwa jambo ilokwishalimua.

Kwa ujumla, mawakili wa Kafulila walisisitiza kwamba mapingamizi yalotolewa na mawakili wa Mhe Hasna na SERIKALI yana lengo la kuhujumu kiujanjaujanja haki kubwa, ya wengi na yenye msingi kwakutumia ufundi kinyume cha masharti ya Katiba.

Baada ya Mjadala huo uliodumu kuanzia satatu asbh mpaka sasaba mchana. Mhe Jaji aliamua kuahirishwa kesi hiyo mpaka a lhamisi asubuhi
 
Huyu Mh. Husna mwilima sasa nimemkumbuka.Mume wake akifanya kazi KLM arusha.Haya tusubiri..lakini Mmmmhhhhhh
 
Hapana Mr Husband wake ni mtu wa dini saana na ni mpole na wala hana makuu.Ni jamaa asiyependa manenomaneno.
 
awike asiwike kutakucha; BI Mwilima kama umefuatilia vzr danadana za uchaguzi wa meya jijini Dsm , basi utakuwa na jibu. muda utaamua
 
Back
Top Bottom