Kesi ya ESCROW kuendelea Mahakama ya Kisutu kesho

Kesi ya ESCROW kuendelea Mahakama ya Kisutu kesho

chuuma

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
363
Reaction score
557
KESI YA MAFISADI WA ESCROW, PAP, IPTL NA SINGASINGA SETHI DHIDI YA MHE KAFULILA WAKITAKA KAFULILA AWALIPE 100M KUENDELEA KISUTU KESHO.

Kesi hiyo No 239 of 215 iliyofunguliwa na Kampuni za IPTL,PAP na Mkurugenzi wa PAP Bw Singh Sethi itaanza kuunguruma kesho Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mchauru baada ya pande mbili kushindwa kukubaliana nje ya mahakama( mediation) kufikia May9.2016.

Kesi hiyo ilifunguliwa upya Mahakama ya Kisutu baada ya kufunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salama, kesi No 110 ya 2014 ambayo ilitupwa kutokana na hoja kwamba madai walalamikaji kuwa walipwe fidia ya 310bn kama fidia ya kuchafuliwa na Mhe Kafulila nje ya Bunge kuonekana ni madai ya jumla na hivyo Mahakama Kuu haiwez kushughulikia madai ya jumla isipokuwa Mahakama za chini.

Nikawasababu hiyo, walalamikaji waliamua kuifungua kesi hiyo Mahakama ya Kisutu na kupunguza madai kutoka 310bn waliokuwa wamedai Mahakama Kuu hadi 100m ambayo wameomba kulipwa Mahakama ya Kisutu.

Walalamikaji kwa upande wao wanawakilishwa na Wakili Makandege wakati upande wa mlalamikiwa Mhe Kafulila anawakilishwa na Wakili Mtobesya na Masawe.

Katika hatua nyingine, Mawakili wa Mhe Kafulila wameingiza leo Mahakamani nyaraka za aina 6 ambazo wamepanga kuzitumia katika kesi hiyo kuthibitisha madai ya Mhe Kafulila dhidi ya walalamikaji kuwa walipora mabilioni kwenye akaunti ya tegeta escrow kifisadi, Nyaraka hizo ni; Mkataba wa IPTL vs Tanesco wa mwaka 1995, Mkataba wa Tegeta Escrow wa 2006, Ripoti ya Ukaguzi maalumu wa CAG kuhusu miamala ya Tegeta Escrow ya 2014, Ripoti ya PAC yenye maazimio ya Bunge ya Novemba 2014, Uamuzi wa awali wa Mahakama ya Benki ya dunia wa Feb12,2014 pamoja na Hukumu ya Mahakama hiyo ya Benk ya dunia ilotolewa Septemba 2016.

Katika hatua nyingine, Mhe Kafulila kupitia mawakili wake amepanga kuiomba Mahakama ielekeze ripoti ya uchunguzi wa PCCB kuhusu ufisadi huu iwasilishwe mahakamani pamoja na ripoti ya Baraza la Maadili iliyoendesha mashtaka kuhusu sakata hili na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Rais nayo yaletwe Mahakamani ili kuthibitisha ukweli wa jambo hilo.
 
Bunge liliishia wapi na hili sakata? Sasa kama mahakama zetu zinauwezo wa kuendesha kesi na madai ya aina hii, mahakama ya mafisadi inakazi gani? Yaani hii nchi raha sana, wametupiga pesa, wakawagawia wakubwa pesa, wakubwa wakatukejeli pesa za mboga na wengine wakajiita nyoka wa makengeza, kuna watu wakaitwa tume ya maadili wakakaidi (Hata sijui lile zoezi liliishia wapi) kana kwamba haitoshi, Tanescoimeamriwa kulipa pesa hizohizo kwa benki ya standard chartered. Bado tanesco wameonyesha nia ya kuongeza bei ya umeme 18% mapema 2017.

Funga kazi, wamefungua kesi ya kudai fidia, seriously?
 
Kati ya vitu vinavyoniuma ni huu mzimu escrow.....

Kiukweli Kikwete hapa uliwakamua watanzania.....

Milioni 400 kupitia IPTL per day kuna watu hawana huruma kabisa na nchi......
 
Bila watanzania kujitambua kashfa juu ya kashfa zitaendelea tuu tutaishia kubishana hapa watu wanapiga madeal tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom