Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Shahidi wa kumi na moja, David Mwanaya kutoka Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi, juzi aliieleza Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inayosikiliza kesi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, kuwa alikuta shati lenye matone ya damu walipofanya upekuzi nyumbani kwa mshtakiwa wa sita, Abdallah Petro, eneo la Kilimahewa, Ilemela, mjini hapa.
Akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Robert Kidando, shahidi huyo alidai walizikuta kofia mbili za jeshi hilo moja ikiwa na nembo nyeupe na nyingine nyeusi.
Mbele ya Jaji Sirilius Matupa anayesikiliza kesi hiyo ya mauaji namba 192 ya mwaka 2014, shahidi huyo ambaye ushahidi wake ulisitishwa baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi dhidi ya maelezo ya mshtakiwa wa pili, Chacha Mwita,aliyeomba kuviwasilisha mahakamani kama vielelezo, alidai pia walikuta sime, mtarimbo, tindo, simu aina ya Nokia na picha mbili za mtuhumiwa akiwa amevaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi huku ameshikilia bunduki aina ya Shotgun Greener.
Hata hivyo, kabla ya kukabidhi vielelezo hivyo mahakamani, upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili James Njelwa, ulipinga ukidai havikuorodheshwa kwenye orodha ya vielelezo ambavyo vinaelezwa vitakuwa 12 bila kufafanua ni vya aina gani.
Hoja hiyo ilizua malumbano ya kisheria kati ya upande wa mashtaka na utetezi, ambao hatimaye walimwomba Jaji Matupa kuwapa muda wa dakika 10 kujadiliana na waliporejea hawakuwa na suluhu.
Kutokana na pande hizo kutopata suluhu, Jaji aliamuru vielelezo hivyo vipokelewe kwa sababu upande wa utetezi uliokuwa ukipinga ulishindwa kutaja vifungu vya sheria vilivyokiukwa ili kuiongoza Mahakama kutoa uamuzi.
Baada ya uamuzi huo wa Jaji, mawakili wa utetezi walipata fursa ya kumhoji shahidi huyo.
Mahojiano kati yake na Wakili Njelwa yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili: Katika ushahidi wako wa awali, ulisema mshtakiwa wa pili (Chacha Mwita) hajui kusoma na kuandika, sasa alijuaje kuwa hiyo ni bunduki ya Shortgun Greener na namba zake?
Shahidi: Hiyo namba kuikariri ni rahisi, hata mtoto wako ambaye hajui kusoma na kuandika anakariri kukuzidi wewe, pia inaonekana ile bunduki walikaa nayo muda mrefu, hivyo jina alikuwa ameshalikariri.
Wakili: Alikwambia waliompiga risasi huyo mzee aliyekuwa kwenye gari walikuwa wangapi?
Shahidi: Alisema walikuwa wengi ila aliyepiga risasi ni mmoja tu, Muganyizi.
Wakili: Wakati unamhoji mtuhumiwa, ulimuuliza anataka kutumia lugha gani?
Shahidi: Sikumuuliza kwa sababu niliona anazungumza vizuri lugha ya Kiswahili
Wakili: Je ulimpa chai mtuhumiwa kabla ya kumhoji?
Shahidi: Sikumpa na hiyo siyo kazi yangu.
Wakili: Kwenye hizo karatasi, tunaona ulipomaliza kuandika maelezo yake na muda uliorekodi chini ya maelezo katikati, lakini ulipoanza kuandika maelezo muda uliandika nje ya mstari pembeni, siyo kwamba ulifanya hivyo ili baadaye umuongezee maneno ambayo hakuyasema?
Shahidi: Siyo kweli, Jeshi la Polisi huo ndiyo utaratibu wake na ndivyo tulivyofundishwa hata ukienda mbinguni tunaandika hivyo.
Wakili: Ungependa ushahidi wako uliotoa hapa mahakamani uaminiwe kuliko ule aliotoa Afande Konyo?
Shahidi: Usitake kunigombanisha na mkuu wangu wa kazi, vyote viaminiwe.
Awali, akiogozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, shahidi huyo aliyeileza Mahakama jinsi polisi ilivyomtia mbaroni mshtakiwa wa sita, Abdallah Petro akiwa jijini Mwanza na kufanya upekuzi nyumbani kwake, pia alisoma maelezo ya mtuhumiwa wa pili, Chacha Mwita.
Alidai kuwa maelezo hayo yalitolewa na mtuhumiwa wakati akimhoji katika Kituo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Jaji Matupa alimtaka shahidi huyo kuyasoma mbele ya Mahakama maelezo hayo yaliyokuwa na kurasa 16, yaliyomkariri mshtakiwa Mwita akieleza jinsi alivyofahamiana na watuhumiwa wenzake na kushirikiana nao kutekeleza matukio kadhaa ya uhalifu, likiwamo la kumuua Kamanda Barlow.
Jaji: Hebu yasome maelezo hayo mbele ya Mahakama?
Huku akinukuu maelezo ya mtuhumiwa Chacha, shahidi huyo alisoma:
Shahidi: Nilikuwa natafuta nauli ya kwenda Musoma kwa mzazi wangu alikuwa anaumwa, ndipo nilipokutana na Muganyizi (mstakiwa wa kwanza) nikamweleza shida yangu ili amsaidie.
Alinieleza (Muganyizi) nisipate tabu kwa sababu kuna njia rahisi ya kupata fedha kupitia kupora na kuvamia maduka na maeneo ya biashara.
Hivyo, Oktoba 12 mwaka 2012, tulipanga tukutane eneo la Shule ya Msingi Nyakabungo, saa 2:00 usiku ili tupange maeneo na sehemu za kupora. Tulikuwa kundi la watu wengi na kiongozi wetu alikuwa Muganyizi ambaye tulikubaliana kwenda kupora maeneo ya Kilimahewa.
Baada ya Kilimahewa ambako tulivamia na kupora sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye grosery, supermarket na maduka ya simu, Muganyizi aliyekuwa na bunduki aina ya Shotgun Greener yenye namba 13003, alibaki nje kulinda usalama na kuwadhibiti watu wanaosogelea katika kila eneo tulilopora.
Tuliondoka na kuelekea eneo la Kitangiri na tulipofika karibu na Hoteli ya Tai Five, tulikutana na gari aina ya Toyota Pickup ndani lilikuwa na watu wawili, mzee ambaye alikuwa dereva na mwanamke mmoja mweupe.
Tulipolisogelea, Muganyizi ambaye alikuwa kiongozi wetu akamuuliza yule dereva, wewe mzee mbona unatumulika kwa taa, hujui kuwa sisi ni polisi tuko kazini?
Yule mzee naye akatujibu kwa kutuuliza, yaani ninyi hamnifahamu kuwa mimi ni nani, ngoja niwaite polisi.
Baada ya kusema hivyo nilisikia mlio wa risasi, kila mmoja akakimbia, kesho yake nikamtafuta Muganyizi ili anipe fedha zangu, alinipa Sh17,000 tu akidai ndizo fedha tulizopora. Lakini aliniambia inabidi tuuze baadhi ya vitu tulivyopora ili tukimbilie Dar es Salaam, kwa sababu mambo yameshaharibika Mwanza.
Muganyizi aliniambia kuwa tuliyemuua jana yake ni mtu mkubwa na polisi wanaendesha msako mkali hatuwezi kuwa salama tukiendelea kubaki jijini Mwanza. Ndipo tulipokimbilia Dar es Salaama na kukamatwa.
Shauri hilo limeahirishwa hadi kesi hiyo itakapopangwa tena baada ya muda uliopangwa isikilizwe mfululizo kukamilika.
Kwa mujibu wa Jaji Matupa, kesi hiyo ilipangwa isikilizwe mfululizo hadi Machi 25, mwaka huu. Baada ya hapo ataanza kusikiliza mashauri mengine.
Chanzo: Mwananchi